loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Ufaulu juu, wavulana vinara kidato cha 4

UFAULU wa watahiniwa wa shule wa kidato cha nne mwaka 2020 umeongezeka kwa asilimia 5.19 ya mwaka 2019 huku matokeo yakionesha jumla ya watahiniwa 373,958 sawa na asilimia 85.84 ya watahiniwa 434,654 wamefaulu mitihani hiyo.

Akitangaza matokeo hayo jana jijini Dar es Salaam, Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA), Dk Charles Msonde alisema matokeo ya mwaka 2019 ni kwamba watahiniwa 340,914 sawa na asilimia 80.65 ya watahiniwa wa shule ndio waliofaulu mtihani huo na kwa idadi hiyo watahiniwa wa mwaka 2020 ufaulu umeongezeka kwa asilimia 5.19.

Dk Msonde alisema katika ufaulu huo wavulana wameongoza kwa asilimia 86.27 na wasichana asilimia 85.44 na kusema ubora wa ufaulu kwa madaraja kuanzia daraja I hadi la III umeongezeka kwa asilimia 35.10 ikilinganishwa na na mwaka 2019 uliokuwa asilimia 32.01.

Aidha alisema takwimu zinaonesha kuwa watahiniwa wamefanya vizuri zaidi katika masomo ya msingi ambapo ufaulu wa masomo hayo uko juu ya wastani kati ya asilimia 50.53 na 94.83.

Alisema watahiniwa hawakufanya vizuri katika masomo mawili ambayo ni Fizikia yenye asilimia 48.87 za ufaulu na Hesabu ni asilimia 20.12.

“Ubora wa ufaulu kwa kuangalia madaraja waliyopata watahiniwa wa shule unaonesha jumla ya watahiniwa waliopata ufaulu mzuri wa madaraja kuanzia I hadi III ni asilimia 35.10, ufaulu huu umeongezeka ukilinganisha na matokeo ya mwaka 2019 ambayo ufaulu ulikuwa asilimia 32.01 hivyo ubora wa ufaulu umeongezeka kwa asilimia 3.09,” alisema Msonde.

Alitaja watahiniwa 10 bora kitaifa kuwa ni Paul Luziga (Shule ya Sekondari PandaHill-Mbeya), Justina Gerald (Canossa-Dar es Salaam),Timothy Segu (Mzumbe-Morogoro),Isaya Rukumya (Feza Boys-Dar Es Salaam), Ashrafu Ally (Ilboru- Arusha),Samson Mwakabage (Jude-Arusha), Derick Mushi (Iboru-Arusha), Layla Atokwete (Canossa-Dar es Salaam), Innocent Joseph (Mzumbe-Morogoro) na Lunargrace Celestine (Canossa- Dar es Salaam). Shule 10 bora kitaifa ni St Francis Girls (Mbeya), Ilboru (Arusha), Canossa (Dar es Salaam), Kemebos (Kagera), Bethel Sabs Girls (Iringa), Feza Boys (Dar es Salaam), Ahmes (Pwani), St Aloysius Girls (Pwani), Marian Boys (Pwani), St. Augustine Tagaste (Dar es Salaam).

Mikoa mitatu inayoongoza kwa kufanya vizuri ni Arusha, Kilimanjaro na Iringa.

SERIKALI imeiruhusu sekta binafsi kuingiza nchini matrekta madogo ...

foto
Mwandishi: Ikunda Erick

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi