loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Necta: Waliofeli kidato cha pili, la nne kukariri lazima

BARAZA la Mitihani la Tanzania (NECTA) limesisitiza kuwa watahiniwa waliofeli mitihani ya Upimaji wa Darasa la Nne (SFNA) na ya Kidato cha Pili (FTNA) mwaka jana, watakariri madarasa na watalazimika kufanya tena mitihani hiyo wapate fursa ya kuendelea na madarasa mengine ya juu.

Kulingana na taarifa ya matokeo ya mitihani hiyo iliyotolewa jana jijini Dar es Salaam na Katibu Mtendaji wa Necta, Dk Charles Msonde, wanafunzi 203,171 wa darasa la nne na wa kidato cha pili wamefeli.

Kwa mujibu wa Msonde, jumla ya wanafunzi 1,828,268 walisajiliwa kufanya mtihani wa SFNA, lakini waliofanya ni 1,704,404. Kati yao watahiniwa 77 walifutiwa mtihani kwa kubainika kufanya udanganyifu.

Baada ya kutolewa kwa idadi hiyo ya waliofanya udanganyifu, matokeo halali yaliyobaki ni ya watahiniwa 1,704,286 ambayo yanaonesha waliofaulu ni 1,551,599 kwa kupata madaraja kuanzia A,B,C na D na watahiniwa 152,687 wamefeli hivyo watalazimika kukariri darasa hilo.

“Wale wote waliofeli mtihani wa upimaji darasa la nne watalazimika kukariri darasa hilo mwaka 2021, na watakariri na watafanya tena mtihani Novemba mwaka huu na wale watakaofeli tena wataendelea kukariri darasa hilo hadi wafaulu,” alisema Dk Msonde.

Akizungumzia watahiniwa wanaokariri kidato cha pili, Dk Msonde alisema jumla ya wanafunzi 50,484 watakariri kidato hicho mwaka huu na watalazimika kufanya mitihani hiyo na wakifaulu wataendelea darasa lingine na watakaofeli tena wataendelea kukariri kidato hicho.

Akizungumzia idadi ya watahiniwa waliosajiliwa kufanya mitihani hiyo ya FTNA mwaka jana, alisema jumla ya watahiniwa 646,200 walisajiliwa ila waliofanya mitihani hiyo ni 601,948 na kuwa matokeo yaliyotoka ni ya watahiniwa 601,463 huku watahiniwa 63 wakifutiwa matokeo yao kwa udanganyifu na waliofaulu ni 550,979 na waliofeli ni 50,484.

Akitoa tathimini kwa ujumla kwa matokeo ya mitihani hiyo miwili, alisema kwa mitihani ya SFNA, kumekuwa na ongezeko la wanafunzi 20,479 sawa na asilimia 1.34 waliopata fursa ya kuendelea na darasa la tano ikilinganishwa na mwaka 2019.

Aidha, mitihani ya FTNA, Dk Msonde alisema matokeo ya mwaka jana yanaonesha kuwa ufaulu wa mithani hiyo ya kidato cha pili umekuwa asilimia 91.61 ukilinganisha na ufaulu wa mwaka 2019 ambao ulikuwa asilimia 90.04 hivyo mwaka 2020 ufaulu umepanda kwa asilimia 1.57.

SERIKALI imeiruhusu sekta binafsi kuingiza nchini matrekta madogo ...

foto
Mwandishi: Ikunda Erick

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi