loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Simba sasa yageukia Ligi Kuu

MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara Simba wamesema wamesahau michuano ya Kombe la Mapinduzi na sasa wanaelekeza nguvu zao kwenye ligi kuhakikisha wanarudi katika kasi na kufanya vizuri.

Simba ilifungwa na watani zao wa jadi Yanga kwa penalti 4-3 katika mchezo wa fainali uliochezwa hivi karibuni kwenye Uwanja wa Amaan Zanzibar baada ya suluhu ndani ya dakika 90 za mchezo huo.

Kikosi hicho kilirejea Dar es Salaam juzi na kupewa mapumziko wa wiki moja ligi ikiwa imesimama kupisha timu ya taifa iliyokwenda Cameroon kushiriki fainali za Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani (Chan).

Kocha Msaidizi wa Simba, Seleman Matola alisema wanatizama mashindani mengine yaliyoko mbele yao kwa maana ya ligi ya ndani na ile ya Kimataifa kujipanga na kurudi katika kiwango bora.

“Mapinduzi yamepita tunatizama mbele kuona namna tutafanya kwa kurekebisha mapungufu madogo yaliyoonekana, kisha tukirejea wiki ijayo tuanze kujipanga na kufanya vizuri zaidi,”alisema.

Katika michuano ya Mapinduzi, Simba iliwatumia wachezaji waliokuwa hawapati namba kikosi cha kwanza sambamba na baadhi waliokuwa wanawatumia huku wakiwapa mapumziko nyota wao muhimu kama Cletus Chama na Luis Miqquisone na wengine wakiwa katika jukumu la timu ya taifa.

Matola alisema yapo baadhi ya makosa madogo ameyaona atakabidhi ripoti yake kwa uongozi wa klabu hiyo kuyafanyia kazi mapema kabla ya kukutana wiki ijayo kwa maandalizi upya. Kutoka na kasi yao kwenye ligi, mabingwa hao watetezi wanashika nafasi ya pili kwa pointi 35 wakiwa nyuma michezo mitatu dhidi ya anayeongoza Yanga ikiwa na pointi 44.

Iwapo itashinda viporo vyake vijavyo basi upo uwezekano wa kumuondoa Yanga katika uongozi wa ligi pengine kwa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa.

KIKOSI cha Simba cha wachezaji 25 kilitarajiwa ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi