loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wilaya, Jeshi laingilia kati kunusuru waliokumbwa na mafuriko Mtwara

OFISI ya Mkuu wa Wilaya ya Mtwara kwa kushirikiana na Jeshi la Zima Moto na Uokoaji mkoani hapa leo wameanza kuondoa maji eneo la Mchuno katika Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara Mikindani na kuyaelekeza baharini ili waweze kusaidia wakazi wa eneo hilo kurudi katika makazi yao.

Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji na Kamanda wa Zimamoto na Uokoaji Mkoa, Christina Sunga amesema wameanza kuchimba mtaro ambayo utaelekeza maji ambayo kwa sasa yametuama katika makazi ya watu na kuyaelekeza baharini.

“Kutokana na mvua ambazo zilizonyesha kuanzia Januari 10 hadi 13, madhara mbalimbali yametokea hasa katika Manispaa ya Mtwara Mjini makazi mengi yaliingiliwa na maji na kusababisa baadhi ya watu kuhama makazi yao na  juhudi mbalimbali ziliweza kufanyika na hatimaye leo tumeweza kutafuta namna bora ya kuondoa hayo maji ili kuwahakikisha familia zilizoathirika zinarudi katika makazi yao,” amesema.

Kamanda amesema nyumba 217 ziliathirika na mafuriko hayo na kusababisha wakazi hao kuhama na kwenda kutafuta hifadhi kwa jamaa zao na wengine kwenda kwa majirani.

“Athari ambazo pia zimejitokeza ni pamoja na watoto kushindwa kwenda shulen kwa sababu vifaa vyao kama vile nguo za shule zipo kwenye hizo nyuma ambazo zimezingirwa na maji, wakazi walihama makazi yao,” amesema.

Rais wa Zanzibar, Dk Hussein ...

foto
Mwandishi: Anne Robi, Mtwara

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi