loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Umesikia huko? Ferguson amfungukia Henderson

Huenda leo hii angekuwa nyota wa muda mrefu ndani ya Manchester United, lakini timu ya madaktari ilishauri kuachana na nahodha huyo wa Liverpool kwa sababu staili yake ya kukimbia ilidhihirisha ni kiungo ambaye pengine angeandamwa na majeraha.

Taarifa ikufikie kuwa nyota wa Liverpool, Jodan Henderson kama sio madaktari kumshauri aliyekuwa kocha wa Man United, Alex Ferguson huenda leo tungeshuhudia akikipiga Old Trafford.
 
Akizungumza na mtandao wa Sky Sport Fergie amesema “Tulikuwa tayari kumsajili Henderson kutoka Sunderland, nilizungumza na Steve Bruce ( Kocha wa zamani Sunderland ) kwa bahati mbaya idara yetu ya matibabu ikashauri staili yake ya kukimbia ingeweza kumletea shida.”
 
Ferguson ambaye alistaafu kuifundisha United msimu wa 2013, amesema ingekuwa kazi bure kama angemsajili Henderson halafu asipate nafasi ya kucheza kutokana na majeraha hata hivyo ameongeza kuwa alihuzunika kumkosa mwingereza huyo.

 

KOCHA wa Tottenham Spurs, Jose Mourinho amesema kwamba kila kitu ...

foto
Mwandishi: MANCHESTER, England

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi