loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Serikali kusogeza vituo vya utalii kwa wananchi

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Damas Ndumbaro amesema kuwa Serikali ipo katika mkakati maalum wa kuvitawanya vivutio vya utalii ili kuvileta karibu na watu hivyo kufanya watanzania wengi zaidi waweze kufanya utalii wa ndani kitu kitakachochea ukuaji wa uchumi.

Ndumbaro amebainisha hayo leo alipokuwa akizungumza na mwandishi kwa njia ya simu na kusema kuwa kwa miaka mingi sasa vivutio vingi vya utalii hapa nchini viko katika mikoa michache, huku Arusha ikiwa maarufu zaidi.

“Uwepo wa vivutio vingi vya utalii katika sehemu moja inawapa ugumu   watu walio mbali na mkoa huo kufika kufanya utalii wa ndani, kwa mfano wale wanaotokea katika mikoa ya Kagera, Simiyu au Mwanza” amesema Dk Ndumbaro.

Amesema wanataka kuongeza vivutio vya utalii kote nchini ili watu walio karibu na vivutio husika wasiende mbali kufanya shughuli za utalii.

Rais wa Zanzibar, Dk Hussein ...

foto
Mwandishi: Alfred Lukonge

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi