loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mtaturu aweka mbele elimu

Mbunge wa Singida Mashariki, Miraji Mtaturu  amesema kipaumbele chake cha kwanza jimboni humo ni kuhakikisha kila mtoto anapata elimu kwakuwa elimu ndio msingi wa maendeleo kwenye kada yoyote hapa nchini.

 Mtaturu amesema hayo jimboni humo alipokuwa anatoa vifaa mbalimbali vya masomo kwa wanafunzi 1161 wanaotoka katika familia zisizo na uwezo.

 “Serikali yetu imewekeza katika elimu ambayo kwa sasa ni bure   na mimi kama mbunge naunga mkono jitihada hizi za serikali kwa kutoa vifaa vya shule ili kisiwepo kikwazo chochote kwa watoto ambao wazazi wao hawana uwezo” amesema Mtaturu.

 Vifaa alivyotoa mbunge huyo ni pamoja na sare za shule, madaftari pamoja na kalamu vyenye thamani ya shilingi milioni 30.

Rais wa Zanzibar, Dk Hussein ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi