loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wafurahishwa na uwajibikaji wa UWATA

WAKAZI wa Halmashauri ya Manispaa ya Tabora waliojiunga na Umoja wa Wanatabora (Uwata)  wameanza kufaidi matunda ya umoja huo baada ya kuanza kumilikishwa viwanja na kupewa hati zao pasipo usumbufu.

Wakizungumza na gazeti hili kwa nyakati tofauti baadhi ya wanachama wamesema umoja huo umekuwa mkombozi kwa wakazi wa manispaa hiyo kwani kila aliyekamilisha taratibu za kujiunga amekabidhiwa kiwanja na hati.

Mkazi wa manispaa hiyo, Kessy Abdulrahman aliyejiunga na umoja huo mwaka juzi pia ni diwani wa kata ya Gongoni alisema kuwa umoja huo umewarahisishia kupata viwanja na kuomba mikopo ya ujenzi kutoka benki.

Alisema kuwa tangu kuanzishwa kwake mwaka 2018 wananchi wengi wamejiunga na kupatiwa viwanja vya kujenga nyumba za makazi na wale wasio na uwezo wa kujenga chama kimeingia mkataba na benki kwa ajili ya kuwezeshwa mikopo nafuu ya ujenzi.

Kessy alibainisha kuwa kutokana na manufaa hayo wakazi zaidi ya 1,500 wameshajiunga na umoja huo na wengine wameendelea kukamilisha taratibu za kujiunga ili kumilikishwa viwanja vyao na kupewa hati na Bima ya Afya.

Mwenyekiti wa umoja, Othman Mango alisema umoja huo umekuwa msaada mkubwa kwa wakazi wa manispaa hiyo kuwezeshwa kupata ardhi, alibainisha malengo yao makuu kuwa ni kuharakisha maendeleo ya wananchi.

Alieleza kuwa kupitia umoja huo wamekusudia kuanzisha Mji wa Kisasa  katika manispaa hiyo hivyo wote wanaojiunga na umoja huo watapewa viwanja ili kujenga makazi yao katika eneo hilo ambalo tayari limeshatengwa na kupimwa kisheria.

Alifafanua kuwa eneo hilo litakuwa na huduma zote za kijamii na nyumba zitakazojengwa zitakuwa za kisasa ili kulifanya kuwa eneo la kipekee lenye mandhari ya kuvutia.

Alisisitiza kuwa kila mwanachama atapewa kiwanja kilichopimwa kisheria na kumilikishwa kuepusha migogoro ya ardhi na kuwa chanzo cha mapato ya ardhi kwa halmashauri ya manispaa hiyo.

Mango alisema kuwa umoja huo utanufaisha wakazi wote wa manispaa hiyo wakiwemo wahindi, waarabu na makabila mengineyo kwani watapata huduma zote stahiki kwa ustawi wa kijamii.

DAKTARI bingwa wa magonjwa ya moyo katika Taasisi ...

foto
Mwandishi: Lucas Raphael, Tabora

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi