loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mtoto aua baba, dada kwa kisu naye afa kwa kupigwa mawe

KIJANA mwenye umri wa miaka 32 mkazi wa Nyasaka B jijini Mwanza, anadaiwa kumuua baba na dada yake kwa kuwachoma kwa kisu na kisha yeye kuuawa kwa kipigo kutoka kwa majirani.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Mwanza, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza, Jumanne  Mliro alimtaja  muuaji huyo kuwa ni Richmond Benet (32)  ambaye alikuwa akiishi nyumbani kwa baba yake ambako pia dadake huyo alikuwa akiishi.

Alisema tukio hilo la mauaji ni la Januari 15 saa 9 mchana katika eneo la Nyasaka B ,Manispaa ya Ilemela.

Kwa mujibu wa kamanda, kijana huyo alianza kumchoma kisu baba yake mzazi, Benet Ntulanabo (66) ambaye alikuwa Mchungaji wa Kanisa la Yesu lililopo Buhongwa, jijini Mwanza. Kisha alimchoma kisu dada yake,Renata Benet (42)

Kamanda  Mliro alisema uchunguzi wa awali umeonesha kuwa kijana huyu hakumaliza masomo yake katika Chuo Kikuu cha Kampala kilichopo Gongolamboto, Dar es Salaam.

Alisema tangu aliporudi nyumbani hapo, alikuwa akiishi katika mazingira ambayo yalikuwa hayaeleweki, yaliyowatia hofu ndugu na wazazi wake.

“Baada ya kutenda tukio na kelele kusikika wananchi walijitokeza na mtuhumiwa alitoa nje akaendelea kutishia watu wengine na kutishia kutaka kuwachoma visu lakini walimrushia mawe, na kumdhibiti na polisi wakaongeza nguvu wakamkamata,” alisema.

Kamanda alisema lakini kijana huyo alikuwa katika hali mbaya hivyo alikimbizwa katika hospitali ya rufaa na kabla hajapatiwa matibabu alipoteza maisha.

Muliro alisema polisi  inaendelea na uchunguzi kubaini chanzo cha tukio hilo.

 

 

DAKTARI bingwa wa magonjwa ya moyo katika Taasisi ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu, Mwanza

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi