loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Takukuru yarejesha nyumba iliyopokwa na mikopo umiza

TAASISI ya Kuzuia  na Kupambana na Rushwa ( Takukuru) wilayani Kahama mkoani Shinyanga  imerejesha  nyumba ya  familia ya Edward  Mpolosi iliyokuwa imechukuliwa  kinyume  cha utaratibu na mfanyabiashara  wa mkopo umiza,  Masero Nyamhanga.

Kaimu mkuu wa Takukuru  wilaya ya Kahama,  Frank Masilamba  aliwaambia waandishi wa habari jana kwamba utaratibu uliotumika  kujimilikisha  nyumba hiyo iliyokuwa katika kitalu J 165 mtaa wa Nyihogo  haukuzingatia sheria.

Masilamba alisema kuwa nyumba hiyo inarejeshwa kwa familia ya  marehemu Edward Mpolosi  aliyechukua mkopo wa Sh 300,000 lakini alipochelewesha  kulipa deni hilo liliongezeka   riba hadi kufikia Sh milioni 10.5.

"Mkataba uliofanyika, sisi Takukuru tumechunguza na kuona ni batili  kwa mauziano ya nyumba  hiyo huku mkopeshaji akijua  wazi kuwa alikuwa anatenda  kosa kinyume na sheria za ukopaji "alisema Masilamba.

Masilimba  alisema kuwa  watoto wa marehemu  walifika katika ofisi za Takukuru kueleza namna ya mkopo ulivyofanyika  dhidi ya marehemu baba yao na  mfanyabiashara huyo  na kuona namna alivyodhulumiwa  nyumba lakini walianza uchunguzi  na kubaini kuwa makubaliano ya mauziano ya nyumba  hiyo yalikuwa  ni batili.

Mkuu wa wilaya ya Kahama, Anamringi Macha  alisema kuwa serikali imeamua  kuikabidhi nyumba hiyo kwa watoto wa marehemu ambao ni Rose na George  waendelee kuimiliki baada ya mfanyabiashara   ambaye  alimkopesha fedha baba yao  kukosa uhalali wa umiliki.

"Hatuta wavumilia  wafanyabiashara  wanaotumia fedha zao kunyanyasa wananchi wanyonge kwa kuwakopesha mikopo umiza  ambayo imekuwa  ikiendelea  kupoka haki za watu wengine na tutaendelea kuwakamata nakuwachukulia hatua pindi tukiwabaini"alisema Macha.

Rose Edward  ambaye alikabidhiwa nyumba hiyo na mkuu wa wilaya  alishukuru  serikali   kwa hatua hiyo.

 

DAKTARI bingwa wa magonjwa ya moyo katika Taasisi ...

foto
Mwandishi: Kareny  Masasy, Kahama

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi