loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mradi  wa kutumia michezo kuboresha elimu wazinduliwa

SERIKALI imewataka wadau wa maendeleo wenye nia ya kusaidia na kutoa michango yao kwenye sekta ya elimu kutoa kipaumbele katika uimarishaji wa miundombinu ya kujifunzia na kufundishia ambayo ni changamoto kubwa kwa sasa kwenye elimu nchini.

Mkurugenzi wa Usimamizi wa Elimu, Ofisi ya Rais Tamisemi, Ally Swalehe alisema hayo juzi kwenye uzinduzi wa mradi  kutumia michezo kuimarisha elimu kwenye shule za msingi zilizopo katika kambi za wakimbizi na wilaya zinazopokea wakimbizi mkoani Kigoma ujulikanao kama Playmaster.

Akizungumza kwa niaba ya Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Swalehe alisema Tanzania sawa na nchi nyingine ulimwenguni inatekeleza malengo ya maendeleo endelevu ya dunia ya mwaka 2030 ambayo lengo la nne ni kuongeza fursa za upatikanaji wa elimu bora kwa misingi ya usawa na ujumuishi ikiwamo kwenye maeneo yenye migogoro na mazingira yanayohitaji misaada ya kiutu.

Alisema serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi wa Rais John Magufuli imeweka sera na kutekeleza mipango mbalimbali ya kuongeza fursa za upatikanaji wa elimu bora kwa kila mtoto wakiwamo watoto wenye mahitaji maalumu .

Hata hivyo alisema ipo changamoto ya uboreshaji wa miundombinu ya kujifunzia na kufundishia hivyo wadau na wahisani mbalimbali wanapaswa kuweka kipeumbele katika kusaidia hilo.

Akizungumzia kuzinduliwa kwa mradi wa Playmaster, alisema kuwa wadau wanaendeleza mahali ambako serikali inatekeleza suala la kutumia michezo kuboresha elimu.

Alisema kutekelezwa kwa mpango kutawezesha kutekelezwa kwa haraka kwa mpango katika maeneo ambayo utekelezaji wake bado upo chini.

Awali akizungumza katika uzinduzi huo, Mratibu wa mradi kutoka Shirika la Uokoaji la Kimataifa (IRC), Andrew Mbega alisema kuwa jumla ya watoto 800,000 wanatarajia kufikiwa wakati wa utekelezaji wa mradi huo wa miaka mitano ambao utatekelezwa kwenye wilaya za Kasulu,Kibondo na Kakonko mkoani Kigoma.

Mbunge wa Musoma Vijijini, Prof  Sospiter Muhongo ameanzisha ...

foto
Mwandishi: Fadhili Abdallah, Kigoma

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi