loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Binti aeleza siri ya kupasua kidato 4

MMOJA wa wasichana bora katika matokeo ya Kidato cha Nne mwaka 2020, Rose Kaale (15) ameeleza siri ya mafanikio kitaalumu akisema sehemu kubwa imetokana na ushirikiano wa wazazi,walimu na yeye binafsi.

“Shuleni kulikuwa na ushindani, kila mwanafunzi anasoma kwa bidii na kila mmoja alikuwa anataka afaulu sasa hiyo pekee inakufanya nawe usome,lakini pia mazingira ya kujifunzia shuleni ni mazuri na walimu walitutia moyo na kutufundisha kwa juhudi,”alisema Rose.

Alisema alitegemea kufaulu ingawa hakufahamu kama atakuwa miongoni mwa wanafunzi bora kitaifa.  Alisema matokeo yamezidi kumtia moyo kuendelea kusoma kwa bidii ili kupata matokeo mazuri zaidi kwa lengo la kutimiza ndoto yake ya kuwa miongoni mwa wachumi bora duniani.

“Nilisoma kidato cha kwanza hadi cha nne Shule ya Sekondari  Precious Blood ya Arusha, nilisoma masomo ya biashara na nikafaulu vizuri kwa kupata daraja la kwanza, napenda kuendelea kidato cha tano kwenye shule yenye mchepuo wa biashara kwa masomo ya Uchumi,Biashara na Uhasibu (ECA)”,alisema Rose.

Alisema anapenda kuwa mchumi au mhasibu kwa sababu mama yake mzazi, Rose Melkior Mrema ni mhasibu na  ndiye anayemvutia  kupenda fani hiyo.Rose anashauri wanafunzi wengine kusoma kwa bidii, kutokata tamaa.

Mama Mzazi wa Rose, Rose Mrema alisema amefurahi kwa mtoto wake kupata daraja la kwanza na kuwa miongoni mwa wanafunzi bora kitaifa na kuwa hiyo imetokana na juhudi binafsi na na ushirikiano wa shule na wazazi.

“Rose amefanya vizuri, ni mtoto mwenye akili ila sikuwaza kama angekuwa miongoni mwa wanafunzi bora kitaifa, anapenda sana kusoma vitabu anaweza kusoma kitabu kimoja kwa siku mbili na akakielewa chote, ana vitabu vingi tofauti vya maarifa na ujuzi, ambavyo nimemsadia kuongeza ufaulu huo.

Mama huyo alisema, imefikia mahali sasa hana sehemu ya kuhifadhi vitabu na badala yake wamemnunulia kifaa kama kompyuta mpakato kiitwacho Candle ambacho kina vitabu aina zote .

“Mtoto wetu  Rose anapenda kusoma na hivi anajaribu kutushawishi tukamsajili  kusoma mitihani maalum ya uhasibu(CPA), tumemwambia asubiri kwanza aende kidato cha tano na sita alafu akienda chuo ndio atajiunga, ila bado hajatuelewa,”alisema Mama mzazi wa Rose, Rose Mrema.

Rais wa Zanzibar, Dk Hussein ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi