loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Serikali yaonya uanzishaji maabara bila kibali

SERIKALI imesema hairuhisiwi mtu yoyote kuanzisha huduma ya maabara bila kuwa na kibali.

Agizo hilo imetolewa na Msajili wa Maabara Binafsi kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wzee na Watoto, Dominic Fwiling'afu wakati wa kikao cha pamoja na wasajili wa bodi na mabaraza ya kitaaluma kutoka wizara hiyo jijini Dodoma.

Fwiling’afu alizielekeza maabara binafsi zote kubandika vibali vya usajili wa maabara eneo la mapokezi ili mtu yoyote anayeingia kupata huduma kwenye maabara aweze kuviona na kuthibitisha kuwa maabara hiyo inatoa huduma kisheria.

Aidha, aliagiza leseni za watumishi wa maabara zibandikwe pia ili mtu anayehitaji au kufika kupata huduma avione.

“Sheria yetu namba 10 ya  1997 pamoja na kanuni yake ya 2005 zinatoa maelekezo thabiti kabisa ya namna ya usajili, namna gani ya kuendesha huduma hizi na inatoa katazo kupitia kifungu chake cha 14 na 15 mtu yoyote uruhusiwi kuanzisha huduma hii bila kusajiliwa na usajili unatolewa na bodi ya maabara binafsi Tanzania,” alisema.

Alisema wamekuwa wakishirikiana na watendaji kuanzia ngazi ya chini ya kata hadi juu, na kuwa wanajua katika ngazo ya kata ndio zinaanzisha maabara hizo hivyo watendaji wa kata wakijua ni maabara gani imeanzishwa na kama wana mashaka nayo wanaweza kutoa taarifa wizarani basi itakuwa rahisi kuzimalia maabara bubu.

DAKTARI bingwa wa magonjwa ya moyo katika Taasisi ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Maalumu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi