loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Naibu Waziri aifagilia TMA

NAIBU Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Godfrey Kasekenya, ameipongeza Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) kwa ufanisi na utendaji mzuri wa kazi zao kiasi ambacho taifa linatambuliwa na Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) na shughuli zake kutegemewa na nchi za jirani.

Kasekenya aliyasema hayo alipofanya  ziara yake katika ofisi za mamlaka hiyo kujionea shughuli na majukumu ya TMA  katika ofisi kuu za mamlaka hiyo zilizopo Jengo la Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam na  kupokea taarifa ya utendaji na kuzungumza na menejimenti ya TMA.

“Kwanza niwapongeze sana kwa kazi nzuri mnayoifanya, sasa endeleeni kuboresha zaidi. Kimsingi nimefarijika sana kusikia Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dk Agness Kijazi pia ni Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) hii ni hatua kubwa. Kutambulika kwa Dkt. Kijazi kimataifa ni sifa kwa taifa letu hivyo nawapongeza sana,” alisema.

Alibainisha kuwa amesikia Tanzania, imepewa jukumu na Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) kusaidia mataifa takribani matano jirani na nchi katika masuala ya  hali ya hewa hii pia ni sifa kwa taifa na kuonesha  kukubalika.

Aliitaka TMA kutambua mchango wa wafanyakazi wanaofanya vizuri na hata kuwapongeza na wale wasiowajibika kuwawajibisha ili kuongeza ari ya utendaji ndani ya mamlaka.

Pia TMA ihakikishe taarifa zake zinasaidia katika ujenzi wa miundombinu nchini na pia kuwa na utaratibu mzuri wa kuziifadhi kisasa ili ziendelee kulisaidia taifa leo na hata hapo baadaye zitakapohitajika.

Katika hatua nyingine, Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Kasekenya ameviomba vyombo vyote vya habari nchini kusaidia kusambaza taarifa za hali ya hewa zinazotolewa na TMA kwa wananchi ili ziweze kuwasaidia wananchi kujua na kufuata ushauri wa mamlaka.

Alisema licha ya mamlaka hiyo kuchakata taarifa nzuri za hali ya hewa itakuwa kazi bure kama hazitawafikia wananchi mapema kwa ajili  ama kujihami au kujipanga kulingana na ushauri wa wataalam hao.

Awali Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dk Agness Kijazi alisema viwango vya utoaji wa taarifa sahihi vya TMA vimeendelea kuboreshwa mwaka hadi mwaka na kuishukuru serikali kuongeza vifaa na wataalam pamoja na kuwaongezea ujuzi kielimu mara kwa mara.

Mbunge wa Musoma Vijijini, Prof  Sospiter Muhongo ameanzisha ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi