loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

EPZA wakumbushwa kujenga maeneo mengine ya viwanda

WAZIRI wa Viwanda na Biashara, Geoffrey Mwambe ameiagiza Mamlaka ya Maeneo Maalumu ya Uwekezaji kwa Mauzo ya Nje (EPZA) kujikita katika ujenzi wa maeneo mapya ya viwanda kulingana na biashara iliyopo katika mkoa husika kwa kuanzia na mikoa ya Lindi, Mtwara na Pwani kwa ajili ya kuwawezesha wajasiriamali wadogo kuchakata korosho ikifuatiwa na maeneo mengine yayozalisha pamba kwa wingi pamoja na uchenjuaji madini

Alisema hayo alipokuwa akizungumza na menejimenti na wafanyakazi wa EPZA alipofanya ziara katika taasisi hiyo akiambatana na Naibu Waziri wa Viwanda Exaud Kigahe  pamoja na baadhi ya wakurugenzi wa Wizara ya Viwanda na Biashara.

Waziri Mwambe pia aliiagiza  EPZA kuyaendeleza na kuyatunza maeneo yote inayoyamiliki ambayo imeshayalipia kwa ajili ya ujenzi wa viwanda pamoja na kufuatilia madeni yote inayowadai wapangaji wake ili fedha hiyo itumike katika kuendeleza maeneo ya viwanda na kufikia malengo iliyojiwekea ambayo hayajafikiwa hadi sasa.

Aliwaasa  watumishi wa EPZA kufanya kazi kwa weledi, uadilifu na kuepuka vitendo vya rushwa wanapowahudumia wafanyabiashara pamoja na kujieendeleza katika taaluma zao ili kuendana na wakati,  kutoa huduma bora katika wigo mpana wa biashara na kuongeza idadi ya wafanyabiashara  wanaowahudumia.

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara alisisitiza EPZA kuyaendeleza maeneo inayoyamiliki ili kuepusha migogoro ya ardhi na wananchi wanaovamia maeneo hayo pamoja na kutunza maeneo  kwa ajili ya ujenzi wa viwanda kwa kizazi kijacho.

Mbunge wa Musoma Vijijini, Prof  Sospiter Muhongo ameanzisha ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi