loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Jafo aamuru viongozi miradi ya TBA wakamatwe

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Suleiman Jafo ameamuru kukamatwa na kuwekwa ndani kwa viongozi na wasimamizi wa miradi ya Wakala wa Majengo nchini (TBA) kwa kuchukua kiasi kikubwa cha fedha wakati miradi iliyotolewa fedha utekelezaji wake umekwama.

Jafo alisema hayo wilayani Uvinza mkoani Kigoma alipokuwa akikagua miradi mbalimbali ya ujenzi ikiwemo nyumba ya Mkuu wa Wilaya Uvinza, nyumba za watumishi na hospitali ya wilaya Uvinza.

Akiwa wilayani Uvinza, Jafo alielezwa taarifa kuwa TBA ilichukua kiasi cha Sh milioni 500 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya Mkuu wa Wilaya Uvinza miaka mitano iliyopita lakini hadi sasa nyumba hiyo imefikia usawa wa msingi.

Waziri Jafo pia alionesha kukerwa kutokana na kukwama kwa jengo la Utawala la Halmashauri ya Wilaya Uvinza ambapo kiasi cha Sh  milioni 900 kimetolewa lakini mradi umekwama kwa miaka zaidi ya mitatu na sasa ujenzi upo usawa wa madirisha.

Akitoa taarifa kwa Waziri Jafo, Meneja wa miradi ya ujenzi katika ofisi ya Mkuu wa mkoa Kigoma, Masawika Kachenje alisema kuwa miradi hiyo ilianza mwaka 2013 na ilipaswa kukamilika mwaka 2018 na waliomba pesa kwenye miradi hiyo Kama malipo ya awali.

“Tumehangaika na TBA kuona wanatekeleza miradi lakini bado utekelezaji umekuwa mgumu kwa sababu fedha zimeenda TBA makao makuu, wakati kuna miradi fedha hazipelekwi na hivyo miradi imekwama, tumeshavunja mikataba yote na tumewaandikia tangu mwaka 2019 fedha zirudishwe lakini hadi sasa hakuna utekelezaji uliofanyika,” alisema Machenje.

Mkuu wa wilaya Uvinza, Mwanamvua Mrindoko alimueleza Waziri Jafo kuwa analazimika kuishi kwenye nyumba za kontena zilizoachwa na mradi wa ujenzi wa barabara za kiwango cha lami wa Kidahwe hadi Uvinza kutokana na kukwama kwa ujenzi wa nyumba ya Mkuu wa wilaya.

Mrindoko alisema kuwa wamefanya jitihada kuhakikisha TBA wanarejesha fedha lakini bado hazijarejeshwa.

Kutokana na hali hiyo Waziri Jafo aliagiza kuorodheshwa kwa miradi yote iliyokwama mkoa wa Kigoma ambayo ilikuwa inatekelezwa na TBA, kueleza thamani ya kazi iliyofanyika na kiasi cha pesa kilichopelekwa na taarifa hiyo iwasilishwe ofisini kwake aweze kuifanyia kazi.

DAKTARI bingwa wa magonjwa ya moyo katika Taasisi ...

foto
Mwandishi: Fadhili Abdallah, Kigoma

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi