loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mangungu, Nkamia kuchuana Simba Na Mwandishi Wetu

WAGOMBEA Murtaza Mangungu na Juma Nkamia wamepitishwa kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa Simba katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Februari 7, mwaka huu kuchukua nafasi ya Sued Nkwabi ambaye alijiuzulu Septemba 14, mwaka jana baada ya kuhudumu kwa takribani miezi kumi pekee.

Akizungumza Dar es Salaam jana Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Simba, Boniface Lihamwike alisema walianza mchakato wa uchaguzi Desemba 13 mwaka jana na jumla ya fomu 11 zilichukuliwa lakini zilizorudishwa ni saba pekee.

‘Waliorudisha fomu ni Hassan Dalali, Juma Nkamia, Rashid Shangazi, Mohamed Soloka, Murtaza Mangungu, Wakili Omar Tika na Piton Mwakisu lakini baada ya kuyapitia tulipitisha majina matano,” alisema

Alisema majina yaliyopita Shangazi, Mangungu, Nkamia, Wakili Tika na Mwakisu baada ya Soloka na Dalali kukosa sifa kutokana na kanuni na vigezo na katiba ya Simba.

Pia alisema wagombea wanne waliwekewa pingamizi isipokuwa Mangungu lakini walishinda mapingamizi hayo na wakati mchakato ukiendelea Mwakisu aliandika barua ya kujitoa lakini wiki hii pia wagombea wawili pia walijitoa.

“Wagombea Rashid Shangazi na Wakili Hamis Tika wameandika barua ya kujiondoa hivyo kwa sasa wagombea ni Juma Nkamia na Murtaza Mangungu,” alisema Lihamwike.

Aidha alisema kampeni zitafanyika kwa siku na kuwaasa wagombea kufanya kampeni za kistaarabu kwa kufuata katiba ya Simba na kuahidi kusimamia uchaguzi huru, wa wazi  na wa haki.

KIKOSI cha Simba cha wachezaji 25 kilitarajiwa ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi