loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

JPM: Limeni kwa wingi mazao ya chakula, hakuna Corona

RAIS John Magufuli ametoa wito kwa Watanzania kuzitumia mvua zinazonyesha nchini kote kulima kwa wingi mazao hasa ya chakula kwa kuwa yatahitajika kwenye nchi ambazo wananchi wake wamefungiwa kutokana na ugonjwa wa covid-19 unaosababishwa na virusi vya corona.

Rais Magufuli ameyasema hayo leo kwenye ziara yake wilayani Muleba, Mkoani Kagera na kuwataka watanzania kumtukuza na kumshukuru Mungu kwa Baraka zake kwa Taifa kutokana na kuliepushia janga la Corona ilihali ugonjwa huo ukiendelea kusababisha vifo vya maelfu ya watu katika nchi nyingine Duniani.

Amesema  kuepushwa na janga hilo watanzania wanatakiwa kuchapa kazi hasa kuzalisha mazao mbalimbali yakiwemo ya chakula kwa ajili ya kuzisaidia nchi ambazo zinashindwa kufanya uzalishaji.

“Sasa hivi mvua zinanyesha katika maeneo mbalimbali ya nchi yetu, nawaombeni sana ndugu zangu Watanzania tulime mazao hasa ya chakula, tulime kwa wingi ili baadaye tuje kuwasaidia wenzetu ambao wanashindwa kulima kutokana na Corona”, amesema  na kuongeza

“Mvua zinanyesha ni Baraka kwetu, Mungu ametuokoa na Corona, nchi zinazotuzunguka mpaka Ulaya watu wanakufa na Corona, kuna taaarifa ya habari nilikuwa naisikiliza kuna nchi watu 1,500 wamefariki kwa siku, sisi hatufi, maana yake Mungu ametupenda, Mungu ametulinda.

“Mvua zinazoendelea kunyesha kote nchi tuzitumie kwa kulima Migomba, tulime Viazi, Uwele wakati zikiisha sisi tunavuna na kuwauzia waliojifungia ndani. Barabara nzuri hata ukilima Matikiti magari yatasafirisha vizuri bila shida.” amesema
 

Rais wa Zanzibar, Dk Hussein ...

foto
Mwandishi: Vicky Kimaro

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi