loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

DC apiga marufuku biashara ya nguruwe

MKUU wa Wilaya ya Kahama, Annamringi Macha amepiga marufuku biashara ya nyama ya nguruwe na nguruwe wenyewe baada ya wanyama hao kukumbwa na homa ya nguruwe (African Swine Fever).

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake juzi, mkuu huyo wa wilaya alisema  amechukua uamuzi huo ili kuwakinga wananchi na watumiaji wa kitoweo hicho na madhara ya ugonjwa huo.

"Maeneo yanayofanya biashara ya nyama ya nguruwe, machinjio, wapishi na sehemu za starehe haziruhusiwi kufanya biashara hiyo kwa sasa mpaka itakapotangazwa tena," alisema Macha.

Alisema dalili za mlipuko wa ugonjwa huo zilianza Desemba mwaka jana na sasa unaonesha kusambaa.

Inaelezwa kuwa hadi sasa 500 wamekufa kutokana na ugonjwa huo katika mazizi matano ya wafugaji wa wanyama hao wilayani humo.

Ugonjwa huo ambao hauna kinga ulishawahi kutokea kipindi cha mwaka 2007.

Macha pia alipiga marufuku usafirishaji wa wanyama hao kutoka sehemu moja kwenda nyingine bila kibali cha daktari na atakayekiuka agizo la serikali hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.

Daktari wa Mifugo Halmashauri ya Mji wa Kahama, Dk Damian Kilyenyi amethibitisha kuwa zaidi ya nguruwe 500 wamekufa kwa ugonjwa huo.

Alisema hatua zilizotangazwa na mkuu huyo wa wilaya ni muhimu ambazo wao kama wataalamu wanazishauri kwa mamlaka ili kuzuia kusambaa kwa ugonjwa huo na kuhatarisha maisha ya walaji na wananchi wengine.

Mmoja wa wafugaji kutoka kata ya Mhongol, Kishiwa Amos  alisema nguruwe akikumbwa na ugonjwa huo anaanguka na kufa ghafla na kuiomba serikali kufanya jitihada za makusudi kuutokomeza.

BENKI ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) imepongeza uthubutu ...

foto
Mwandishi: Kareny Masasy, Kahama

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi