loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Jaffo akerwa uchafu kukithiri Kigoma Ujiji

HALI mbaya ya uchafu katika  Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji imemkera Waziri wa Tamisemi, Suleiman Jaffo na kumtaka mkurugenzi wa manispaa hiyo, Mwailwa Pangani na watendaji wake kujitafakari.

 

Jaffo alitoa kauli hiyo alipotembelea sehemu ya kumwagia uchafu (Dampo) unaozalishwa katika manispaa hiyo kupitia mradi unaotekelezwa kwa mkopo nafuu kutoka Benki ya Dunia.

Jaffo alielezwa kuwa licha ya dampo hilo kukamilika halmashauri haina uwezo wa kuzoa takataka kusafisha mji wake.

 

Hata hivyo, waziri huyo alisema haiingii akilini kuona kiasi kikubwa cha fedha kinatumika kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo lakini halmashauri inashindwa kuzoa takataka.

"Kigoma Ujiji ni moja ya miji 45 nchini ambayo karibu itaanza kutekeleza mpango wa ujenzi wa barabara za kiwango cha lami katika barabara zake zote hivyo siyo suala la masihara kuona mji una lami kila mahali lakini uchafu unazagaa kila mahali, hatutakubali ni lazima mjitafakari na kuweka mpango wa kukabiliana na hali hii," alisema Jaffo.

Meya wa Manispaa ya Kigoma Ujiji, Baraka Lupoli alimweleza Jaffo kwamba hali ya uzoaji uchafu katika manispaa hiyo ni mbaya kwani ni idadi ndogo tu ya takataka zinazozalishwa ndizo zinazozolewa hivyo kufanya mji kuzagaa uchafu.

 

Alisema baada ya Baraza la Madiwani kuanza kazi lilimtaka  mkurugenzi na wakuu wa idara kuhakikisha suala la usafi wa mji linazingatiwa hasa uzoaji wa takataka.

 Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma Ujiji, Pangani alikiri kwamba uzoaji tataka na usafi wa mji huo ni tatizo kubwa na kueleza kwamba hali hiyo inatokana na kutokuwapo kwa bajeti kwa ajili ya uzoaji takataka licha ya kukamilika kwa dampo hilo.

 

Alisema kwa muda mrefu hakukuwa na fungu maalumu lililotengwa na halmashauri kwa ajili ya uzoaji takataka na badala yake fedha zilikuwa zikitolewa kwenye vifungu vingine hasa mafuta kwa ajili ya gari za kubebea takataka.

Mbunge wa Musoma Vijijini, Prof  Sospiter Muhongo ameanzisha ...

foto
Mwandishi: Fadhili Abdallah,Kigoma

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi