loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Chikwende aahidi raha Simba

MSHAMBULIAJI mpya wa Simba, Perfect Chikwende amesema atajitahidi kwa uwezo wake kuonesha kiwango katika timu yake hiyo mpya kuhakikisha wanapata matokeo mazuri.

Chikwende alisajiliwa juzi kabla ya kufungwa kwa dirisha dogo la usajili kwa mkataba wa miaka miwili akitokea FC Platnum ya Zimbabwe.

Akizungumza Dar es Salaam mchezaji huyo alisema ana furaha kujiunga na Simba na kuahidi mashabiki kuwa atafanya kazi kwa bidii ili kuisaidia timu kufikia malengo iliyojiwekea.

“Najua Simba ni timu kubwa na nzuri nina furaha kujiunga nao, nitajitahidi kwa uwezo wangu kujituma kwa kufanya kazi kwa bidii timu ipate matokeo,”alisema.

Mchezaji huyo alisema anaamini akicheza mashindano mengi yatasaidia kuimarisha kiwango chake.

Kwa upande wa Kocha Msaidizi wa Simba Selemani Matola alisema Chikwende ni mchezaji mzuri walimuona katika michezo miwili waliyocheza na FC Platnum, ambapo Simba ilishinda jumla ya mabao 4-1.

“Chikwende ni mchezaji mzuri tumemuona katika mechi mbili za Ligi ya mabingwa, nafikiri atatusaidia. Ni vizuri kumsajili mchezaji mnayemuona,”alisema.

Uongozi wa klabu hiyo ulisema usajili wa mchezaji huyo ni kutaka kuboresha kikosi chao katika harakati za kutetea taji la Ligi Kuu sambamba na michuano ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika.

Anatarajiwa kujiunga na wekundu hao hivi karibuni kwa maandalizi ya mechi zijazo mara tu baada ya kumalizika kwa michuano ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani (Chan) inayoendelea huko Cameroon.

MSANII bora wa kike, Zuhura Othman Soud au Zuchu amefunguka ...

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi