loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Ruvu yaongeza watano, yapania nne bora

TIMU ya Ruvu Shooting imeboresha kikosi chake kwa kusajili wachezaji watano wapya huku msimu huu ikipania kumaliza Ligi Kuu Tanzania Bara ndani ya nne bora.

Aidha, timu hiyo leo inatarajia kuingia kambini tayari kwa maandalizi ya mzunguko wa  pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara ulioanza hivi karibuni, lakini umesimama kupisha mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (Chan).

Akizungumza na gazeti hili jana Msemaji wa Ruvu Shooting, Masau Bwire alisema usajili wa wachezaji hao umezingatia mapendekezo ya benchi la ufundi linaloongozwa na Kocha Mkuu Charles Mkwasa.

Aliwataja wachezaji waliosajiliwa kuwa ni Edward Manyama kutoka  Namungo, Haji Mwinyi kutoka KMKM ya Zanzibar, James Msuva kutoka KMC, Adam Kyondo kutoka Yanga na Haruna Fadhili kama mchezaji huru kila mmoja akisaini mkataba wa miezi sita.

“Tayari tumekamilisha usajili wa dirisha dogo na sasa tunaelekeza nguvu katika maandalizi ili kikosi kirejee kwa nguvu mpya na kufanya vizuri mzunguko wa pili,”alisema.

Alisema malengo waliyojiwekea ni kuhakikisha wanapambana kama sio kuchukua ubingwa basi angalau wamalize katika nafasi nne za juu.

Bwire alisema yote hayo yanawezekana kama wataendelea na morali yao waliyokuwa nayo tangu mzunguko wa kwanza.

Ruvu kwa sasa inashika nafasi ya tano kwenye msimamo ikiwa na pointi 28 baada ya kucheza michezo 18 na kati ya hiyo kushinda saba, kupata sare saba na kupoteza mitatu.

KIKOSI cha Simba cha wachezaji 25 kilitarajiwa ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi