loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Waitara ataka Morogoro wajenge dampo la kisasa

NAIBU Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mwita Witara, ameiagiza Halmashauri ya Morogoro kujenga dampo la kisasa katika eneo lingine na kuweka usimamizi mzuri wa taka.

Waitara alitoa agizo hilo baada ya kutembelea dampo lililopo eneo la Viwandani katika manispaa hiyo na kukuta hali ya usimamizi wa taka isiyoridhisha.

Alisema hali katika dampo hilo si nzuri kutokana na kutokidhi vigezo vya dampo vikiwemo kutokuwa na utaratibu wa kutenganisha aina za taka ili kuwa na usimamizi mzuri.

“Hapa hakuna usimamizi mzuri, hatuwezi kuwa na dampo la aina hii na ni ngumu kudhibiti taka hapa. Kama mlivyosema, mmetenga eneo la ekari 174, nawahimiza muandike andiko mpate fedha mjenge dampo la kisasa; hapa hapafai na si rafiki kwa mazingira haya maji yakisambaa ni hatari kwa binadamu, wanyama na mazingira,” alitadharisha.

Naibu waziri huyo alisisitiza elimu kutolewa hususan kwa vijana kutumia fursa ya taka zinazooza ili kujiajiri kwa kutengeneza mbolea ya mboji kwa ajili ya shughuli za kilimo na bidhaa nyingine.

Awali akizungumza katika kikao na maofisa mazingira wa mkoa, manispaa na kata kilichofanyika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Waitara alielekeza kila shule ya msingi na sekondari kusimamia kila mwanafunzi apande mti.

“Naelekeza wakurugenzi wote wa wilaya na watu wa mazingira kwenye mikoa na wilaya kuhakiksha kila mwanafunzi anapanda mti. Mwanafunzi  wa shule ya msingi autunze kwa miaka saba na kwa yule wa sekondari atautunza kwa miaka minne awapo shule, hili litasaidia si tu katika kutunza mazingira, bali pia kupata vivuli na matunda,” alisema.

Aidha, Waitara aliwataka maofisa mazingira kuzitembelea klabu za mazingira zilizopo katika shule mbalimbali ili kutoa hamasa kwa wanafunzi wanaounda klabu hizo kuendelea kushiriki katika utunzaji mazingira.

Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Bakari Msulwa, alisema mikakati iliyowekwa wilayani humo ni kuelekeza kila mwanafunzi anayeanza shule akishirikiana na mzazi wake, kupanda mti mmoja na kuutunza.

Msulwa alisema kwa wastani kila shule inapokea wanafunzi takriban 200, hivyo wanaamini watapata idadi hiyo ya miti na kuwa kwa kufanya hivyo watasaidia kampeni ya kupanda miti kushika kasi.

DAKTARI bingwa wa magonjwa ya moyo katika Taasisi ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Maalumu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi