loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Waziri: Wahitimu CBE msibweteke

WAZIRI wa Viwanda na Biashara, Geoffrey Mwambe amewataka wahitimu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) kutobweteka na kiwangho cha elimu walichopata, badala yake wahakikishe wanajiendeleza katika ngazi mbalimbali za elimu.

Aidha, amekitaka chuo hicho kuweka mpango wa kutoa elimu ya biashara kwa maofisa biashara wa halmashauri zote sambamba na mkakati wa namna ya kukuza ujasiriamali nchini.

Alitoa ushauri huo katika Mahafali ya 13 ya CBE Kampasi ya Mwanza alipowasisitiza wahitimu wakiwamo wenye astashada, kutoridhika na kiwango chao cha elimu na badala yake, walenge kufikia ngazi ya stashahada huku wenye stashahada wakilenga kufikia ngazi ya shahada.

 

Aliwataka pia wahitimu kutumia utaalamu walioupata chuoni hapo kutatua changamoto mbalimbali za jamii likiwamo tatizo la ukosefu wa ajira. 

Waziri Mwambe alitaka mashirika binafsi na ya serikali kupelekeka wafanyakazi katika chuo hicho ili wapate elimu na ujuzi utakawwezesha kutenda kwa ufanisi zaidi.

Katika mahafali hayo, Waziri Mwambe alikishauri CBE kufungua kampasi katika maeneo ya Nyanda za Kaskazini na Kusini kwa ajili ya wananchi wa mikoa ya Ruvuma, Lindi na Mtwara na akasema serikali itaendelea kushirikiana na chuo hicho kuboresha miundombinu ya elimu katika kampasi zake.

Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Kampasi ya Mwanza, Profesa Emmanuel Mjema, alisema katika mahafali hayo kuwa, wanafunzi 447 walihitimu katika ngazi mbalimbali.

Alisema CBE kipo mbioni kuanzisha kozi mpya ya Stashahada ya Masoko na Utalii sambamba na mkakati wa kuanzisha kampasi katika Mkoa wa Iringa na Zanzibar.

Profesa Mjema aliipongeza serikali kwa kuongeza bajeti ya mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu hali iliyokinufaisha chuo hicho na wanafunzi wake.

BENKI ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) imepongeza uthubutu ...

foto
Mwandishi: Alexander Sanga, Mwanza

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi