loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

JPM: Tanzania haitishwi wala haibabaishwi

RAIS John Magufuli amempa tano Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Balozi  David William Concar na kuwataka mabalozi wengine nchi kujifunza kwake kwa kuwa Tanzania haitishwi wala haibabaishwi na yeyote.

Rais Magufuli ameyasema hayo leo na kudai kuwa ni balozi pekee ambaye hajamuona akiandika kwenye mtandao wa twiter  zaidi ya kufanya kazi.

“Wewe ni wa kipekee, sijawahi kukuona ‘ukitwiti’ zaidi ya kufanya kazi, nenda kawafundishe na wenzako namna ya kufanya kazi na Tanzania. Tanzania ni nchi ambayo haitishwi wala haibabaishwi na yeyote, inafanya kazi zake kwa kujiamini,” alisema na kuongeza:

“Ukizungumza na Uingereza mwambie Waziri Mkuu ninamualika aje kututembelea, lakini aje na misaada mingine, mgeni njoo mwenyeji apone.”

BENKI ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) imepongeza uthubutu ...

foto
Mwandishi: Vicky Kimaro

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi