loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Ujumbe wa EU wavutiwa uchaguzi ulivyofanyika

MKUU wa Ujumbe wa Jumuiya ya Ulaya (EU) nchini Uganda, Balozi Atillio Pacifici amesema wamevutiwa kwa jinsi uchaguzi mkuu Rais na wabunge ulivyoofanyika kwa mpangilio mzuri na amani wiki iliyopita.

Mkuu huyo wa ujumbe wa EU alisema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika viwanja vya Kololo ambako kulikuwa na kituo cha Tume ya Uchaguzi  cha kutangaza matokeo ya uchaguzi wa ubunge kwa tarafa tano za Kampala.

"Tumeona jinsi uchaguzi ulivyoendeshwa vizuri na kwa utaratibu watu wakisubiri kupiga kura na kila kitu kilifanyika kwa amani sana.”

“Tumevutiwa sana, maofisa wa Tume ya Uchaguzi walikuwa na na weledi mkubwa. Inafurahisha kulikuwa na  vijana wengi na raia wa Uganda wasomi walioshiriki mchakato wa uchaguzi," alisema Balozi Pacifici wakati alipotembelea  kituo hicho cha kuhesabia kura.

Hata hivyo, EU haikutuma watazamaji wa uchaguzi huo kama kawaida yake inavyofanya katika sehemu mbalimbali kunakofanyika uchaguzi mkuu kutokana na  serikali kutotekeleza baadhi ya  mapendekezo ambayo watazamaji wa umoja huo waliyatoa wakati wa uchaguzi mkuu uliopita.

Badala yake, EU ilituma watu wanaowaita watazamaji wa kidplomasia ambao ni wanadiplomasia kutoka balozi mbalimbali za nchi wanachama kutazama mambo yanavyotendeka katika uchaguzi huo.

WABUNGE wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EALA) wameridhishwa ...

foto
Mwandishi: KAMPALA

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi