JESHI la Kujenga Taifa (JKT) limesitisha kwa muda mafunzo ya kujitolea ya jeshi hilo kwa mwaka 2020/2021 kwa sababu za ndani ya jeshi hilo.
Kaimu Mkuu wa Utawala JKT, Kanali Hassan Mabena alisema hayo leo na kwamba vijana wote waliokuwa wamechaguliwa kwa ajili ya kuhudhuria mafunzo ya kujitolea watarejeshwa majumbani.
Kanali Mabena amewataka vijana ambao wamechaguliwa lakini hawajaripoti wasiende kuripoti kambini mpaka hapo itakapotangaziwa tena.