loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

SMZ yataka huduma bora uwanja wa Karume

WAZIRI wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Rahma Kassim Ali ameagiza huduma za watalii katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume ziboreshwe zaidi ili kwenda na kasi ya kuingia wageni msimu wa watalii.

Amesema Zanzibar inapokea watalii wengi ambapo kwa wiki moja ni zaidi ya wageni 6,000 kutoka katika mabara yote ya dunia, hivyo ni muhimu kwa uongozi wa uwanja huo kujipanga kuwahudumia.

''Nimefurahishwa kwa kiasi fulani kuona baadhi ya kasoro nilizoziona wiki mbili zilizopita zimerekebishwa, hata kwa upande wa watendaji wa idara ya uhamiaji wameongeza kasi ya kutoa huduma za ukaguzi wa hati za kusafiria kwa watalii,'' alisema Rahma.

Uongozi wa uwanja huo ulimweleza waziri huyo kuwa kasoro zilizokuwa zikijitokeza katika uingiaji wa wageni zimeanza kufanyiwa kazi na idadi kubwa ya watalii sasa wanawasili visiwani humo.

Meneja wa uwanja huo, Haji Makame alisema hayo wakati akitoa taarifa kwa waziri huyo aliyekuwa katika ziara ya kuangalia shughuli za kuingia kwa wageni wakiwemo watalii na huduma wanazopatiwa uwanjani hapo.

Alisema wameongeza utoaji  huduma kwa wageni ikiwamo  kuongeza madirisha sita yanayohudumia watalii kwa wakati mmoja na kupunguza muda wa kukaa foleni kupata huduma.

Alisema huduma nyingine zimeimarishwa vikiwamo vipimo muhimu kama chanjo  ya kujikinga na maradhi ikiwamo covid-19.

''Kwa ufupi tumeongeza rasilimali watu katika utoaji wa huduma mbalimbali katika uwanja huu kipindi cha mwezi huu ambapo tumekuwa tukipokea idadi kubwa ya watalii kutoka Ulaya,'' alisema Makame.

Naye Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari Masoud Sururu alisema kasi ya kuhudumia watalii imeongezeka kwa kuongeza wafanyakazi hivyo kupunguza msongamano na foleni za wageni.

 

''Tumeongeza wafanyakazi wengi zaidi katika kutoa huduma kwa wageni na hivyo kupunguza foleni na msongamano wa watalii pamoja na huduma za viza mtandao zimerahisisha mambo mengi,'' alisema.

Katika kipindi hiki ambacho baadhi ya nchi za Ulaya zinakabiliwa na maambukizi ya corona, Zanzibar imekuwa ikipokea watalii wengi wanaokwenda kwa ajili ya mapumziko kutoka katika bara la Ulaya Magharibi, Russia na Poland.

Rais wa Zanzibar, Dk Hussein ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi