loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wazazi walalamika kutoona matokeo mitihani kidato cha 4

WAZAZI wa wanafunzi waliofanya mitihani ya taifa ya kidato cha pili (FTNA) na mtihani wa taifa wa kidato cha nne (CSEE) mwaka jana katika Shule ya Sekondari Geita Islamic Seminary wamelalamika kutoona matokeo ya mitihani ya watoto wao.

Shule hiyo yenye namba ya usajili S 4829, mwaka jana ilikuwa na wanafunzi 41 waliosajiliwa kufanya mtihani wa taifa wa kidato cha nne na wengine 14 waliosajiliwa  kufanya mtihani wa kujipima wa kidato cha pili, ambao wote walifanya malipo ya fedha za mitihani hiyo.

Hali hiyo inaelezwa kusababishwa na Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Joas Jasson kuchelewa kuwasilisha malipo ya fedha zilizotolewa na wanafunzi hao katika sehemu husika.

Taarifa zinaonesha kuwa, wanafunzi wa kidato cha pili walilipia Sh 25,000 kila mmoja, huku wa kidato cha nne wakilipa Sh 50,000 kila mmoja na kufanya jumla ya malipo ya wanafunzi 55 kuwa Sh milioni 2.4 zilizopokelewa na mwalimu mkuu huyo.

Mbali na wanafunzi wa shule hiyo kueleza kufanya malipo ya fedha za mitihani hiyo kwa wakati lakini matokeo yaliyotangazwa wiki iliyopita na Baraza la Mtihani la Taifa (NECTA), wazazi wa wanafunzi hao wamelalamikia kutoona matokeo ya watoto wao hadi sasa.

Kwa mujibu wa vyanzo vya ndani kutoka shuleni hapo, mwalimu mkuu huyo alipokea fedha zote kabla ya muda wa mwisho uliopangwa na Necta kufanya malipo lakini alifanya malipo akiwa amechelewa ingawa hakuna uhakika kama aliziwasilisha kwenye akaunti husika.

Akizungumza juzi na waandishi wa habari, mkazi wa mtaa wa Mkoani, wilayani Geita, Salima Francis ambaye mtoto wake amehitimu wa kidato cha nne shuleni hapo, alisema ameshangazwa kutoona matokeo ya mwanaye wakati hakuna anachodaiwa ikiwamo ada ya shule na fedha za mtihani na alifanya malipo yote kwa wakati.

"Sisi tumeshangazwa matokeo ya watoto wote yametoka lakini matokeo ya watoto wetu Geita Islamic hayajatoka, nimejaribu kumtafuta mwalimu hapatikani mpaka Jumamosi alipopatikana akasema anafuatilia matokeo yatoke lakini mpaka leo (juzi) matokeo hayajatoka.

Mzazi mwingine, Masumbuko Lwakubamwa alisema ametazama mtandaoni matokeo ya mwanaye lakini hajayaona.

Alipotafutwa na HabariLEO Mwalimu Mkuu wa shule hiyo ambaye anadaiwa kuchelewesha malipo ya fedha hizo, alisema naumwa baada ya kupata ajali  baiskeli kuahidi kuwa akimaliza kupata tiba atawasiliana na  mwandishi kwa ajili ya ufafanuzi.

Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Shule ya Geita Islamic, Juma Nkya alisema wamefuatilia suala hilo na wameambiwa na mamlaka husika wawasilishe risiti za malipo hivyo wanafanya mchakato wa kupata risiti hizo na iwapo hawataziona shule itawajibika kulipia kwa mara ya pili ili kuondoa utata uliopo.

Rais wa Zanzibar, Dk Hussein ...

foto
Mwandishi: Yohana Shida, Geita

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi