loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Biden aanza na Trump

Rais wa Marekani, Joe Biden ameanza kazi kwa kishindo mara baada ya kuapishwa hapo jana kwa kutengua sera kadhaa muhimu za Donald Trump aliyemuachia ofisi.

 Baada ya kiapo Biden alinukuliwa katika akaunti yake ya Twitter akibainisha kuwa “Hakuna muda wa kupoteza linapokuja suala ya kushughulikika masuala ya dharula yanayogusa maslahi ya taifa letu”.

Moja ya vitu ambavyo Rais huyo mpya wa taifa hilo lenye nguvu kubwa ya kiuchumi duniani anataka mchakato wake uanze mapema ni mapambano dhidi ya ugonjwa wa Corona, sera mpya ya mabadiliko ya tabianchi na masuala ya uhamiaji akitaka kufanya tofauti na utawala wa Trump ulivyokuwa unashughulikia mambo hayo.
 
Biden aliapishwa hapo jana kuwa rais wa 46 wa taifa hilo sherehe ambazo mtangulizi wake Donald Trump alisusia kushiriki akitoa kisingizio kuwa uchaguzi uliomwingiza madarakani kiongozi huyo mpya haukuwa halali.

PAPA Francis ameanza ziara yake ya ...

foto
Mwandishi: WASHINGTON DC, Marekani 

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi