Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Seif Khamis Gulamali amempongeza Waziri wa Nishati na Madini, Dk Medard Kalemani kwa kasi yake ya kusambaza umeme vijijini.
Gulamali amesema hayo Jijini Dodoma kwenye Kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini na kubainisha kuwa hadi sasa zaidi ya asilimia 80 ya vijiji vyote hapa nchini vimefikiwa na huduma ya umeme kutokana na jitihada za dhati zilizofanywa na waziri huyo.
“Kasi ya usambazaji umeme vijijini ni kubwa na yawezekana Tanzania ikawa ni nchi ya kwanza Afrika inayoongoza kwenye ufikishaji huduma ya umeme katika maeneo ya vijijini,” amesema Gulamali.