loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Ronaldo sasa mfungaji bora muda wote

Sasa ni rasmi kuwa mtambo wa mabao wa Juventus, Cristiano Ronaldo amekuwa mfungaji bora wa muda wote katika historia ya soka baada ya jana kufunga bao moja katika ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Napoli na kufikisha mabao 760 huku akiisaidia timu yake kuchukua ubingwa wa Italia Super Cup.
 
Ukiwa msimu wake wa tatu tangu alipowasili akitokea Real Madrid ambako alifunga mabao 450, Ronaldo amefunga mabao 85 akiwa na Juventus na mabao 118 Man United, mabao matano akiwa Sporting CP na 102 akiwa timu ya Taifa Ureno.

Nyota wa zamani wa Jamhuri ya Czech, Joseph Bican anabaki katika nafasi ya pili akiwa na mabao 759 akifuatiwa na nguli wa Brazil, Pele mwenye mabao 757.
 
Akiwa Barcelona pekee tangu kuanza soka, Lionel Messi ni mchezaji mwingine ambaye huenda akawa na nafasi kubwa ya kuvunja rekodi ya Pele na Bican ambapo anabaki nafasi ya nne akiwa na mabao 719.

KOCHA wa Tottenham Spurs, Jose Mourinho amesema kwamba kila kitu ...

foto
Mwandishi: TURIN,Italia

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi