loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Ligi Kuu England kama Daladala

Ligi ya Kuu England imekuwa kama Daladala ukishuka mwingine amekaa, suala la kukaa nafasi za juu limekuwa sio inshu kubwa kwani unaweza kukaa kwa masaa tu na ukashuka pengine hata kwa nafasi mbili chini.

Kabla ya michezo iliyopigwa juzi na jana, Man United ilikuwa ikiongoza kwa pointi 37, kabla ya ushindi wa jana wa mabao 2-1 dhidi ya Fulham.

Leicester city juzi iliibamika Chelsea mabao 2-0, hivyo ilipanda hadi nafasi ya kwanza ikiwa na pointi 38, lakini baada ya ushindi wa jana wa Man United dhidi ya Fulham Leicester imeshuka hadi nafasi ya tatu, baada ya Man city pia kushinda dhidi ya Aston Villa

Liverpool ambayo iliongoza kwa wiki kadhaa nyuma sasa imetupwa nafasi ya nne ikiwa na pointi 34 hali ni mbaya zaidi maana katika michezo mitano ya mwisho wameshinda mmoja tu.

Kinachovutia zaidi na kuonyesha ugumu wa ligi hiyo, Man city yenye pointi 38 wana mchezo mmoja mkononi, hivyo kama wakishinda maana yake Man United itabidi arudi nafasi ya pili.

Chelsea iliyowahi kusogea hadi nafasi ya pili sasa inashika nafasi ya nane, mambo yanazidi kuwa magumu maana katika michezo mitano wameshinda mmoja tu nakupoteza mitatu sare moja.

Arsenal ambayo mwezi mmoja uliopita ilikuwa nafasi ya 17, wameanza kujivuta na sasa wanashika nafasi ya 10, ahueni imeanza kuonekana kwa Mikel Arteta baada ya kushinda michezo minne kati ya mitano ya mwisho na kutoa sare moja.

Hiyo ndiyo Ligi Kuu England ukipoteza umepotea

KOCHA wa Tottenham Spurs, Jose Mourinho amesema kwamba kila kitu ...

foto
Mwandishi: LONDON, England

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi