Kocha wa Arsenal, Mikel Arteta amesema kuna haja ya kusajili beki wa kushoto katika dirisha la usajili Januari hii.
Arteta amefikia kutoa kauli hiyo baada ya aliyekuwa mchezaji wa nafasi hiyo, Sead Kolasinac kuicha klabu hiyo na kujiunga na Schalke 04 wiki mbili zilizopita.
Amesema kwa sasa timu hiyo inahitaji mbadala sahihi wa Kieran Tierney anayecheza nafasi hiyo licha ya kuwepo kwa Ainsley Maitland-Niles, Bukayo Saka.