loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Magufuli atuma pole kifo cha Mbunge

RAIS John Magufuli amemtumia salamu za rambirambi Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai, wabunge, wananchi wa Mkoa wa Manyara kutokana na kifo cha Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Mkoa wa Manyara, Martha Umbulla.

Taarifa ya Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Gerson Msigwa, jana ilieleza kuwa, Rais Magufuli amepokea kwa masikitiko taarifa ya kifo cha Mbunge huyo na kwamba pia ametuma rambirambi kwa familia ya marehemu.

 

“Mhe. Martha Umbulla alikuwa mpole, mchapakazi na mpenda maendeleo. Nazikumbuka jitihada zake za uongozi akiwa Mkuu wa Wilaya na akiwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania” alisema Rais Magufuli.

Aliwaomba wanafamilia wawe na moyo wa uvumilivu na ustahimilivu katika kipindi kigumu cha majonzi na amemuombea marehemu apumzike mahali pema peponi.

Taarifa ya Spika wa Bunge, Job Ndugai, iiyotolewa kupitia Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Kimataifa jana ilieleza kuwa Mbunge huyo alifariki dunia akiwa katika matibabu kwenye Hospitali ya HCG Mumbai, India.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Spika Ndugai ametoa pole kwa wabunge wote na wananchi wa mkoa wa Manyara.

Taarifa hiyo ilibainisha kuwa Bunge litashirikiana familia ya marehemu kuratibu mipango ya mazishi na taarifa zaidi zitaendelea kutolewa.

Umbulla alikuwa Mbunge wa Viti Maalumu wa Mkoa wa Manyara. Alizaliwa Novemba 10, 1955. Wakati wa uhai wake pia aliwahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kiteto mkoani Manyara hadi Februari 18, 2015 uteuzi wake ulipotenguliwa.

BENKI ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) imepongeza uthubutu ...

foto
Mwandishi: Magnus Mahenge, Dodoma

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi