loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Washtakiwa 183 wafutiwa mashtaka mkoani Kagera

 
Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) Biswalo Mganga amewafutia mashtaka jumla ya washtakiwa 183 katika magereza ya Karagwe, Bukoba, Biharamulo na Muleba mkoani Kagera.

Mkurugenzi huyo amebainisha hayo wakati akizungumza kwenye hafla ya ufunguzi wa  Ofisi ya Taifa ya Mashtaka wilaya ya Karagwe mkoani Kagera ambapo amesema kuwa mkoa huo unakabiliwa na kesi nyingi za mauaji.

Biswalo ameeleza  baada ya kutembelea magereza mbalimbali  na kuongea na mahabusu walioko ndani ameamua kuwafutia washtakiwa  57 kutoka wilaya ya  Karagwe, 54 Bukoba, 48 Biharamulo  na Muleba 26 huku katika ziara hiyo akikutana na badhi ya washtakiwa ambao ni wahamiaji haramu 15  waliokuwa wamekaribishwa na wazawa wa mkoa wa Kagera. 

"Kimsingi kuna makosa mengi na kesi nyingi ambazo walengwa hawastahili kuwemo gerezani hivyo nimeamua kuwaachia kikubwa niwaombe viongozi wa dini muendelee kuhubiri amani, upendo ili vitamalaki kwani vitasaidia kupunguza hizi kesi,” amesema Mganga. 

Aidha, Biswalo ametanabaisha kuwa hatosita kumchukuliahatua mtu yoyote bila kujali nafasi aliyonayo kisiasa, dini au Serikali ikigundulika kuwa amejihusisha na vitendo vya uhalifu ambapo amesisitiza suala la amani ni jukumu la kila mtu hivyo wanawajibika kuitunza kwa kuepuka kufanya makosa ya jinai.

Kwa upande wake Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Kagera, Ntemi Kilekamajengaamesema mkoa wa Kagera unaongoza kwa kuwa na kesi nyingi za mauaji ambapo amewaomba viongozi wa dini kuendelea kuhubiri amani ili kupunguza vitendo vya uhalifu.

Naye Askofu wa Jimbo Katoliki la Kayanga Almachius Rweyongeza amebainisha kuwa kufunguliwa kwa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka  katika wilaya ya Karagwe kutasaidia wananchi kupata haki kwa wakati sambamba na kuwakumbusha viongozi wenzake wa dini kutimiza wajibu wao wa kuhubiri upendo na amani kwa mujibu wa maandiko matakatifu.

Mwakilishi wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) mkoa wa Kagera, Liberatha Bamporiki ameeleza kufunguliwa kwa Ofisi hiyo ya Mashtaka katika wilaya ya Karagwe kutapunguza gharama na muda mwingi waliokuwa wakiutumia kwenda Manispaa ya Bukoba kufautilia kesi zao.

DAKTARI bingwa wa magonjwa ya moyo katika Taasisi ...

foto
Mwandishi: Mwandishi wetu, Karagwe

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi