loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Dube ataka kujiamini Azam FC

MSHAMBULIAJI wa Azam FC Prince Dube amesema iwapo watajiamini wao wenyewe kama wachezaji na kucheza kwa umoja watafikia malengo yaliyowekwa mwishoni mwa msimu.

Dube ameanza kurejea baada ya kukaa nje kwa miezi miwili akiuguza jeraha la mkono wa kulia aliloumia katika mchezo dhidi ya Yanga Novemba mwaka jana.

Akizungumza kurejea kwake, mchezaji huyo alisema wakifanya kazi kwa pamoja kwa juhudi wanaweza kufanya vizuri na kuisaidia timu kufikia malengo iliyojiwekea.

“Tunahitaji kuendelea kupambana na kujiamini sisi wenyewe kwa kile tunachokifanya, nafikiri tunaweza kufikia malengo,”alisema mchezaji huyo Mzimbabwe.

Alisema amefurahi kupona na kurejea tena katika kikosi atajitahidi kuonesha bidii kuisaidia timu yake kufanya vizuri zaidi.

Dube alionekana kucheza katika michezo ya kirafiki ya Azam FC huko Zanzibar kuonesha kuwa tayari kurejea mzunguko wa pili wa Ligi Kuu soka Tanzania.

Mchezaji huyo alikuwa mwenye kasi katika kikosi hicho baada ya kuifungia timu yake mabao sita na kuchangia pasi nne za mabao kabla ya kuumia.

Huenda sasa kurejea kwake kukarudisha matumaini mapya kwa Azam FC ambayo bado iko katika mbio za ubingwa licha ya kuporomoka kidogo tofauti na alivyoiacha awali.

Azam ipo katika nafasi ya tatu kwa pointi 32 katika michezo 17 iliyocheza ikiwa nyuma pointi 12 dhidi ya kinara Yanga yenye pointi 44 katika michezo 18 na Simba nafasi ya pili kwa pointi 35 katika michezo 15.

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetoa ...

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi