loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Benki ya Ushirika Kilimanjaro tayari kuihudumia Tanzania

BENKI ya Ushirika ya Kilimanjaro imevitaka vyama vya ushirika na watanzania kwa ujumla kujiunga na huduma za benki hiyo ambayo imenuia kuinua uchumi wa Mkoa wa Kilimanjaro na mikoa mingine kupitia vyama vya ushirika.

Hayo yamebainishwa na Meneja Mkuu wa benki hiyo, Godfrey Ng’urah, wakati akizungumza na gazeti hili kwenye ofisi ya Magazeti ya Serikali(TSN) jijini Dar es Salaam alipokuwa kwenye ziara ya kikazi akiambatana na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira.

Alisema benki hiyo imepania kuunganisha vyama vyote vya ushiriki kuanzia vya kahawa,korosho, pamba, katani na vinufaike na uwepo wake.

Alisema kwa kuwa mazao hayo yanayosimamiwa na vyama hivyo ni mengi na yenye kiwango kizuri na kwamba benki inaweza kuvikopesha ili kuviwezesha kufanya kazi zake kwa ufanisi zaidi. Alisema wanufaika pia watakuwa wakulima.

“Benki inaunga mkono harakati za serikali hii inayoongozwa na Rais John Magufuli katika kuhakikisha uchumi wa nchi unaimarika zaidi, na menejimenti imeona kuwa kati ya walengwa ni vyama vya ushirika,”alisema.

Alisema kuviwezesha vyama hivi itasaidia kwa kiasi kikubwa kuinua uchumi kwa kuwa vyama hivi vinafanya kazi na wakulima wa mazao hayo moja kwa moja na benki.

Alisema kuwa pia wanahudumia wananchi mmoja mmoja, vikundi, taasisi na hata mashirika mbalimbali ikiwa ni pamoja na kununua mikopo kwa watumishi wa umma au watu binafsi wenye mikopo benki au taasisi za kifedha.

Alisema mkopo wao ni wa riba ya asilimia 14 unaoweza kulipwa hadi kwa miaka minane. Pia wanatoa huduma za elimu ya biashara na ujasiriamali kwa makundi ya watu kuwaelekeza wanavyoweza kunufaika na mikopo.

Pia alisema kuwa benki hiyo inatoa huduma za mikopo kwa vikundi vya vikoba, saccos na umoja mbalimbali wa wajasiriamali wenye kuhitaji huduma zao.

Alisema kuwa benki hiyo imepewa mtaji wa Sh bilioni nane kutoka benki ya CRDB kwa ajili ya kuimarisha miundombinu ya utendaji na mifumo.

DAKTARI bingwa wa magonjwa ya moyo katika Taasisi ...

foto
Mwandishi: Evance Ng’ingo

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi