loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Kiir ampongeza Museveni urais

Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini ametuma salamu za pongezi kwa Rais Yoweri Museveni kwa kuchaguliwa tena kuongoza Uganda.

Katika salamu zake, Rais Kiir amesema kwa niaba ya watu wa Jamhuri ya Sudan Kusini anampongeza Museveni kwa kuchaguliwa tena kuwa rais wa nchi hiyo ya Afrika Mashariki.

“Ushindi wako unaonesha jinsi raia wa nchi hiyo wanavyokuamini wewe na chama chako cha NRM, hii ni ishara ya shukrani zao kwa juhudi ulizofanya katika kuongoza nchi hiyo katika kipindi cha miaka 34,” alisema Rais Kiir.

Alisema Uganda ni mshirika muhimu katika ukanda wa Afrika Mashariki kiuchumi na imekuwa ikisaidia kuleta amani ya Sudan Kusini.

 “Chini ya uongozi wako, Uganda imebaki kuwa mshirika muhimu wa kikanda katika msaada wa kiuchumi na amani katika eneo hili. Watu wa Sudan Kusini wanashukuru sana kwa mchango wako katika kurudisha amani katika nchi yetu kama mmoja wa wadhamini wa amani," alisema.

 Kiir alimtakia heri Museveni  na kueleza kuwa anatumaini wananchi wa Uganda  watakuwa naye bega kwa bega kuelekea ustawi mkubwa kwa nchi hiyo.

"Nakutakia heri utakapoanza jukumu lako jipya na natumai kuwa Uganda itakubali maono yako na kutembea nawe wakati unapojitahidi kufikia mafanikio zaidi kwa nchi yako,” alisema Rais Kiir.

SERIKALI imeanza mpango wa kitaifa wa ...

foto
Mwandishi: KAMPALA

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi