loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Serikali yapongezwa kuagiza mahakama kupeleka elimu vijijini

SERIKALI imepongezwa kwa hatua yake ya kuiagiza Mahakama Kuu hapa nchini kujikita katika kutoa elimu kwa wananchi waishio vijijini, ambako walio wengi hutatizwa na taratibu za kufungua mashauri.

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Uinjilisti na Elimu wa Kanisa la Evangelist Assemblies of God Tanzania(EAGT)  kanda ya kati, Mchungaji Nason Msanjila .

Akizungumza na waandishi wa habari mkoani Dodoma baada ya Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan kuzindua maadhimisho ya wiki ya sheria nchini na miaka 100 ya mahakama kuu iliyofanyika Dodoma, alisema hatua hiyo ya serikali ya kupeleka elimu kwa wananchi wa vijijini itawasaidia wao kutambua taratibu za kupata haki zao za msingi.

"Ni imani yangu kubwa sasa serikali ikiwapelekea elimu wananchi huko vijijini, wataweza kutambua jinsi ya kufuatilia tofauti na jinsi ilivyo ambapo baadhi yao wanakosa kuzitambua haki zao na kusababisha kutopata haki,”alisema. 

Juzi,  Makamu wa Rais akizungumza kwenye uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya sheria nchini na miaka 100 ya Mahakama Kuu iliyofanyika mkoani Dodoma,aliitaka mahakama kujikita katika mazingira ya vijijini ambako kuna mashauri mengi ambayo hayafiki kwenye vyombo vya sheria huku mengine yakiishia njiani.

Makamu huyo wa Rais alisema kuwa elimu hiyo ikipelekwa vijijini italeta ufanisi na matokeo chanya, hivyo ni vizuri wakapeleka mapendekezo serikalini ya jinsi watakavyoweza kulitatua tatizo hilo la kuwapelekea elimu hiyo watu wa vijijini

Aidha alisema serikali ipo tayari kuungana na mamlaka husika ya mahakama kwa kutambua madhara na unyonge wanaoupata wananchi walio wengi wa vijijini huko ambao hawafahamu taratibu za kimahakama na kusababisha wao kupoteza muda mwingi kufuatilia mashauri,migogoro na kesi na wakati mwingine kujikuta wakikosa haki zao za kimsingi.

SERIKALI imeiruhusu sekta binafsi kuingiza nchini matrekta madogo ...

foto
Mwandishi: Sifa Lubasi

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi