loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Serikali kufuta utitiri mitihani ya majaribio

SERIKALI imekiri kuwapo kwa utitiri wa mitihani ya majaribio kwa wanafunzi wa shule za msingi za umma na binafsi na imesema mitihani mingi haina ubora kwa maendeleo ya kitaaluma ya watoto.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dk Leonard Akwilapo alisema hayo jana na kubainisha kuwa wizara inaangalia uwezekano kuisitisha mitihani hiyo kwa kuwa ni mingi bila sababu za msingi.

“Katika baadhi ya shule, wanafunzi wanawekewa kambi za kila wiki na kufanyishwa mitihani hata wiku za mwisho wa wiki,” alisema Dk Akwilapo wakati wa mkutano wa mwaka unaofanyika kwa siku mbili ulioandaliwa na Tume ya Kikristo ya Huduma za Jamii (CSSC).

Tume imeelezea wasiwasi kwamba kumekuwa na mitihani mingi ya kujitathimini isiyo na ubora. Dk Akwilapo alisema wizara inajua kuwapo kwa mitihani hiyo na kwa sasa inawashirikisha wataalam ndani na nje ya wizara hiyo ili waangalia kuangalia namna ya kuisitisha au kuboresha vipindi.

Alisema kwa mtazamo wake ni kwamba kuboreshwa kwa ufaulu wa masomo kati ya wanafunzi wa shule za msingi na sekondari ni matokeo ya ubora wa ufundishaji na usimamizi wa elimu.

Aidha, Dk Akwilapo ameipongeza Tume ya Kikristo ya Huduma za Jamii (CSSC) kwa kuzingatia matumizi ya teknolojia ya habari na mawasiliano kama njia za kufundishia wanafunzi wa shule za awali na msingi.

“Ninaihakikishia Tume kuwa wizara iko tayari kufanya kazi na tume ili kuimarisha ufundishaji na ujifunzaji kati ya wanafunzi nchini,” alisema Katibu Mkuu.

Tume inasimamia karibu taasisi 1,223 za mafunzo ya elimu inayojumuisha shule za awali 404, shule za msingi 268, shule za sekondari 373, shule za seminari 50, vyuo vikuu tisa vya ualimu, vituo 96 vya mafunzo ya ufundi, na taasisi 22 za elimu ya juu.

Mkurugenzi Mtendaji wa Tume, Peter Maduki alisema shule chini ya Kanisa Katoliki imechukuwa mfumo wa mitihani ya majaribio inayopangwa kwa kusaidiwa na Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA). Maduki alisema mitihani imepangwa katika kila kanda ikihusisha shule za msingi na sekondari.

“Kwa bahati mbaya, kumeibuka mlipuko wa mitihani ya majaribio katika kata na wilaya ambazo ubora wake unatia shaka,” alisema.

Maduki aliishauri serikali kupitia tena mitihani hiyo na kupunguza vipindi ili kutoa nafasi kwa mwanafunzi wa shule za msingi na sekondari kujifunza.

Akizungumzia mkutano huo, Maduki alisema umeandaliwa kama mkakati wa kuwakutanisha wataalamu kutoka wizara za Elimu na Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa zilizopewa jukumu la kusimamia sekta ya elimu.

Tume inatumai mkutano huo utatoa fursa ya kujadili fursa na changamoto zinazoikabili sekta ya elimu ikiwa ni pamoja na kujadili njia bora za kutumia ICT katika ufundishaji na ujifunzaji.

NAIBU Waziri wa Mawasiliano na ...

foto
Mwandishi: Anastazia Anyimike, Dodoma

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi