loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wananchi wapongeza Serikali, TASAC kwa kurahisisha usafiri wa Mafia

“SERIKALI imeokoa maisha ya wananchi wengi wa Mafia, lakini pia imerahisisha shughuli za kibiashara na uchumi kutokana na uwepo wa meli zinazofanya safari zake kutoka Bandari ya Nyamisati, hadi kisiwa cha Mafia, mkoani Pwani,” alisema Abdallah Hussein, mkazi wa Mafia aliyekuwa kwenye Bandari ya Nyamisati akijiandaa na safari ya kwenda kwao Mafia.

Mwananchi huyo alieleza kuwa juhudi za Serikali kupitia Shirika la Wakala wa Meli Nchini (TASAC), la kuhakikisha kuwa safari za majini ni salama, zimechagizwa na kuwepo kwa vivuko vikubwa vilivyo salama lakini. pia uwepo wa bandari imerahisisha shughuli za kiuchumi kati ya maeneo hayo.

Hussein amezungumza hayo punde baada ya Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi  wa TASAC, kutembelea bandari hiyo kujionea shughuli zinazofanyika hususani usalama katika usafirishaji wa abiria na mizigo.

Akizungumza mara baada ya kukagua na kujionea shughuli zinazofanyika kwenye Bandari ya Nyamisati, Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya TASAC, Kapteni Mussa Mandia amesema kuwa serikali  kupitia TASAC itaendelea kuhakikisha safari za majini kote nchini zinakuwa salama na thamani kubwa kiuchumi kwa wananchi.

“ Wananchi wanapaswa kupata huduma bora na salama za majini ili waweze kuendelea na shughuli zao za kiuchumi, TASAC kama chombo cha Serikali kitaendelea kusimamia vyema ili kila kitu kiende vyema,” alisema Kapteni Mandia.

Hata hivyo amewapongeza Mamlaka ya Bandari nchini (TPA) kwa kazi kubwa wanayofanya ya kuhakikisha huduma bora zinakuwepo bandarini hususani uwepo wa mazingira salama.

“Tuna taarifa TPA wamefanya kazi nzuri na wametengeneza bandari nzuri, na hii ni zawadi ya Serikali kwa watu wa Mafia ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakipata changamoto ya usafiri.

“Bandari inapendeza na huduma zinazotolewa ni nzuri. Pia tunawapongeza Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) ambao wamekuwa sehemu ya wanaotoa huduma ya usafiri kwa wakazi wa Mafia.

“Ni kitu cha kipeee na kizuri kwa jeshi kuwahudumia wakazi wa Mafia, wana meli hiyo ambayo imetengenezwa kwa umahiri mkubwa,” alisema.

Kwa upande wake Nahodha wa kivuko binafsi cha MV CAPT 01, Mkanga Suleiman amesema hali ya usafiri kati ya maeneo hayo mawili ni nzuri.

Alisema,“Kwa asilimia 90 hali ya usafiri ni nzuri, huwa  ninahoji wasafiri na wengine wanaeleza jinsi wanavyonufaika, zamani wa usafiri ulikuwa ni wa majahazi, wakati huo ulikuwa unakuta abiria 200 bandarini lakini jahazi lilikuwa linabeba 40 tu.”

Kwa mujibu wa nahodha huyo, gharama ya usafiri kwa mtu mzima ni Sh 21000, watoto chini ya miaka 18 ni 11,000 lakini kwa wale waliochini ya miaka miaka sita ni bure.

SERIKALI imeiruhusu sekta binafsi kuingiza nchini matrekta madogo ...

foto
Mwandishi: Alfred Lasteck, Nyamisati

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi