loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Ng'ombe 200 wakamatwa ndani ya Bonde la Ihefu

Zaidi ya ng'ombe 200  wamekamatwa ndani ya Bonde oevu la Ihefu,  wilayani Mbarali, Mbeya katika operesheni ya kuondoa mifugo katika eneo lililopo ndani ya  Hifadhi ya Ruaha.

Hatua hiyo imefikiwa baada ya Serikali kuagiza  mifugo kuondolewa katika eneo hilo ndani ya siku sita.

Akizungumzia operesheni hiyo, leo , Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila amesema kuwa uharibifu katika Bonde hilo utaathiri mtiririko wa maji katika Mto Ruaha.

 Ameongeza kuwa eneo hilo linachangia asilimia 15 ya maji katika bwawa kuzalisha umeme la Nyerere ambalo bado lipo katika hatua ya ujenzi.

“Nipende kuwaasa wafugaji kiburi na ukaidi sio jambo zuri sana na wasije kuonesha kwamba kuna watu wapo nyuma yao sisi uwa hatuogopi watu bali tunafanya kutokana na taratibu na sheria zilizopo,” amesema Chalamila.

Aidha, Chalamila amekipongeza Chama cha Wafugaji nchini  na hususani wilayani  Mbarali kwa kushirikiana na Serikali katika kutoa elimu kwa wadau wake baada ya agizo la siku sita.

KENYA imetangaza orodha ya nchi ambazo raia wake ...

foto
Mwandishi: Alfred Lukonge

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi