loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Waandishi wahimizwa kushiriki tuzo ya SADC

WIZARA ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kupitia Idara ya Habari-MAELEZO, imetoa wito kwa waandishi wa habari nchini kushiriki tuzo za nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) za mwaka huu.

Wito huo ulitolewa na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO, Rodney Thadeus kupitia taarifa yake kwa vyombo vya habari jana, ambapo alisema tuzo hizo zitatolewa katika maeneo makuu ya uandishi wa habari, magazeti, televisheni, wapiga picha na watangazaji wa redio.

Alisema waandishi wanaotaka kushiriki wanatakiwa kuwasilisha kazi zao kupitia kamati maalumu za tuzo hizo katika nchi husika.

“Kazi za waandishi wa habari za magazeti zitahusisha makala zilizochapishwa katika magazeti, tovuti, majarida zikiwa na maneno yasiyopungua 100 wala kuzidi 2000, kwa upande wa radio kipindi kinatakiwa kisichopungua dakika moja au kuzidi dakika 30 na kiwasilishwe kupitia CD ikiambatanishwa na muswada andishi ili kurahisisha tafsiri  ya kipindi husika,” alisema.

Thadeus alisema kwa upande wa televisheni, washiriki wanatakiwa kuwasilisha kipindi kisichopungua dakika moja au kuzidi dakika 45 na kiwasilishwe kupitia CD kikiambatanishwa na muswada andishi ili kurahisisha tafsiri ya kipindi husika.

Alisema wapiga picha wanatakiwa kuwasilisha picha moja au zisizozidi 20 zilizochapishwa katika toleo moja zikiambatana na nakala ya gazeti husika lililochapisha picha hizo.

Alisema waandishi wa hapa nchini wanatakiwa kuwasilisha kazi hizo Idara ya Habari-MAELEZO Dodoma kwa Mratibu wa Kitaifa wa Masuala ya Habari za SADC, Zamaradi Kawawa kabla ya Februari 28, mwaka huu na kwa waandishi waliopo Dar es Salaam wawasilishe kazi zao katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Mwalimu Nyerere (JNICC).

RAIS wa Zanzibar Dk Hussein Mwinyi ameiagiza  Wizara ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi