loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mwigulu aagiza rasilimali za nchi zilindwe kisheria

WAZIRI wa Katiba na Sheria, Mwigulu Nchemba ameielekeza Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania ifanye utafiti na kupendekeza njia sahihi za kulinda rasilimali za nchi kisheria ili kuondoa mianya ya kuchezewa siku za usoni.

Alitoa agizo hilo jana wakati akizungumza na watendaji wa tume hiyo jijini Dodoma.

Alisema kuna sheria zikiwamo za madini zimerekebishwa kutokana na ujasiri na uthubutu wa Rais John Magufuli kuleta faida kubwa kwa taifa.

"Ni maeneo ambao yalikuwa yanatafuna nchi kwa kiwango kikubwa sana, bila udhubutu wake isingewezekana kufika hatua hii, tusingeweza kuona mabadiliko na maendeleo haya.”

"Ninyi ni mashahidi, kufumua mikataba ile pamoja na sheria ambazo tumezirekebisha, bila uthubutu na maono ya Rais Magufuli ingekuja kama miaka 10 au 20 hivi tusingepata hata mabua maana watu wangekuwa wameshavuna mali zote," alisema.

Nchemba aliitaka tume hiyo kuendeleza juhudi za Rais Magufuli kwa kufanya utafiti na kuangalia upungufu katika  sheria zilizofanyiwa marekebisho na ambazo hazijafanyiwa marekebisho ili wananchi na rasilimali zao walindwe kisheria.

"Tumefanya marekebisho haya kwa nguvu yake na uthubutu wake na utayari wake mwenyewe (Rais Magufuli), sasa nyinyi mlio watafiti lazima muende hatua kubwa zaidi ya hapo ya tutayalindajie na tutayaendelezaje."

“Wanadamu ni wabinafsi na hasa wanasiasa, hivyo tume ina fursa ya kuwasaidia wananchi maisha yao na rasilimali zao vilindwe na sheria. Wananchi wamekuwa na ushahidi kuwa tulikuwa tunaibiwa na zaidi ya Sh trilioni 20 zilizookolewa zimekwenda kwenye maeneo ambayo yanagusa maisha yao moja kwa moja,” alisema. Nchemba.

Aidha, aliitaka tume hiyo ihakikishe sheria hizo zinatafsiriwa kwa lugha ya Kiswahili ili ziweze kujulikana na wananchi wengi.

BENKI ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) imepongeza uthubutu ...

foto
Mwandishi: Anastazia Anyimike, Dodoma

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi