loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

TASAC yaja na mwarobaini wa bandari ‘bubu’

SERIKALI ipo mbioni kurasimisha bandari zisizokuwa rasmi ‘bubu’ ili ziwezo kutoa huduma huku Serikali ikipata kipato chake halali.

Akizungumza baada ya kutembelea gati ya Kilwa Masoko, Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Uwakala wa Meli nchini (TASAC), Kapteni Mussa Mandia alisema tathmini ya awali ilishafanyika na bado inaendelea ya kuona jinsi gani bandari ‘bubu’ baadhi yake zitarasimishwa ili kuongeza ufanisi kwenye shughuli za majini.

 “Kuna changamoto kubwa ya biashara ya magendo, vyombo vya majini visivyokidhi matakwa ya kiusalama lakini pia kumekuwa na uvuvi usiofuta taratibu lakini vyote vinachagizwa na uwepo wa bandari bubu.

 

“Naamini, tutashirikiana na Mamlaka ya Bandari (TPA) sambamba na Serikali za mkoa Tanzania kote kuhakikisha tathmini inakamilika ili baadhi ya Bandari bubu ziwe rasmi ili kunusuru mapato ya serikali na wananchi na wafanyabiashara husika wapate kunufaika.

 “Kama bandari inapokuwa rasmi na kutabulika ni rahisi kuwepo na hali ya usalama kwa wale wanaotumia vyombo vya majini na kwenye Bahari Kuu, usalama wa wananchi pia ni muhimu kwani biashara haramu zinaweza kupenyezwa kupitia bahari kwani ni njia inayotumika na wengi,” alieleza na kuongeza:

 “Kilwa ni eneo lenye historia kubwa, ina gati mbili kuu ambazo ni Kilwa Masoko na Kilwa Kivinjeni… vyote hivi vikiboresha matokeo ya uchumi utokanao na bahari utaongezeka kwa Serikali na watu binafsi.

 Kwa upande wake, Kaimu Meneja Usajili, Ukaguzi na Udhibiti wa Vyombo vya Majini wa TASAC, Mhandisi Alfred Waryana alisema kuwa ni wakati sasa wa Bandari ‘bubu’ na mialo isiyokuwa rasmi kurasimishwa na kupata menejimenti ili vyombo vyote vya majini visajiliwe na udhibiti uwepo ili vinapokuwa majini vinakuwa salama.

 “Tunaamini tunachangamoto kubwa kwenye udhibiti wa vyombo vya majini. Usalama unaanza bandari, lakini tunaona sehemu nyingi bado hazijawa rasmi hivyo tuna kazi ya kubadili hii hali.

 “Mfano, asilimia 70 ya vyombo vya majini kwa upande wa Kusini mwa Tanzania vinapatikana Kilwa lakini baadhi havijasajiliwa lakini pia vinafanya shughuli kwenye bandari zisizokuwa rasmi…

 “… tunatarajia bandari itajengwa na kupitia menejimenti zitakazowekwa, tutajua ubora wa vyombo vilivyopo majini lakini tutahakikisha vyombo vyote vina vifaa vya uokozi,” alisema na kueleza kuwa urasimishaji utakuwa na manufaa kwa Serikali na kwa wananchi vile vile.

 Katika Gati ya Kilwa Kivinjeni, akiwasilisha maombi ya kuwepo bandari kwa serikali, mmoja wa wavuvi katika eneo hiyo, Juma Ngondaye alisema kuwa Serikali imekuwa haifaidiki na gati hiyo kutokana na shughuli nyingi za magendo zinazofanyika.

 “Tunatambua makubwa yanayofanywa na Rais John Pombe Magufuli, tunajua anajua umuhimu wa bandari hapa Kilwa, naamini ikifanyiwa marekebisho na kuwepo kwa mifumo na menejimenti bora ajira zitakuwepo lakini pia Serikali itapata kipato kizuri.

 “Hizi dawa tunazopata hospitalini, watoto wetu wanasoma bure ni matunda ya mifumo rasmi kwenye maeneo mbalimbali. Kama Rais kajenga barabara nyingi, naamini hawezi kushindwa kujenga bandari na serikali kuongeza mapato huku sisi tukipata huduma bora,” alisema Ngondaye.

 

BENKI ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) imepongeza uthubutu ...

foto
Mwandishi: Alfred Lasteck

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi