Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dk Faustine Ndugulile amesema ifikapo mwezi Februari wizara hiyo itatoa tamko kuhusu utapeli wa mitandao na changamoto ya vifurushi.
Dk Ndugulile amebainisha hayo Jijini Dodoma alipokuwa anafungua mkutano uliohusisha wizara hiyo na watendaji waandamizi wa makampuni ya simu hapa nchini.
“Niwatoe hofu watanzania bado tunaendelea na mazungumzo na muda sio mrefu tutakuja na majibu na ufumbuzi wa kina kuhusiana na mambo hayo” amesema Dk Ndugulile.