Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel amesema usambazaji wa chanjo duniani uwe wa usawa.
Akilihutubia Jukwaa la Kiuchumi Duniani jana kwa njia ya video, Merkel amesema jambo la muhimu ni usawa katika utoaji wa chanjo na sio pesa za kuipata chanjo hiyo.
Merkel amesema ni muhimu pia kusaidia upatikanaji wa chanjo kwa mataifa masikini duniani. Tayari nchi zilizoendelea hadi sasa zimeidhinidha chanjo zilizotengenezwa na kampuni katika mataifa ya Magharibi za Pfizer-BioNTech na Moderna.