loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Watatu wakamatwa kwa biashara haramu ya madawa

MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini (DCEA) inawashikilia watuhumiwa watatu kwa kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya aina ya Heroin.

Watuhumiwa hao ni Balozi wa nyumba 50 Mtaa wa Kuwaje Kunduchi jijini Dar es Salaam, Kulwa Pazi (49) maarufu Mama Udodi, Emmanuel Maamuzi (21) na Anachati Mchongeza (20).

Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za kulevya, James Kaji amesema watuhumiwa hao walikamatwa na gramu 400 na Majani makavu ya bangi kete 30.

"Maafisa wa Mamlaka walifanikiwa kukamata kiasi hicho cha dawa zikiwa zimehifadhiwa ndani ya mfuko wa nailoni," amesema Kaji.

Amesema mamlaka inaendelea kuwashikilia watuhumiwa na watafikishwa mahakamani baada ya taratibu za kisheria kukamilika.

Rais wa Zanzibar, Dk Hussein ...

foto
Mwandishi: Vicky Kimaro

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi