loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

TBS yateketeza bidhaa hafifu za mil 40/-

SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) limeteketeza bidhaa zisizokidhi ubora wa viwango zenye thamani ya Sh milioni 40.

Bidhaa hizo zameondolewa sokoni na wakaguzi wa TBS Kanda ya Kati kuanzia Novemba mwaka jana hadi Januari 15, mwaka huu katika mikoa ya Dodoma, Tabora na Singida.

Akizungumza baada ya uteketezaji wa bidhaa hizo katika Dampo la Chidaya, Mkurugenzi wa Udhibiti wa Ubora wa TBS, Lazaro Msasalaga alisema bidhaa zilizoharibiwa ni vipodozi vyenye viambata sumu, vyakula na vinywaji ambavyo muda wake wa matumizi imepita vilivyopatikana katika mikoa mitatu ya kanda hiyo.

“Katika kulinda afya za walaji, TBS tumekuwa tukifanya ukaguzi katika miji yote nchini kupitia kanda zetu sita, na kika wiki tunafanya ukaguzi na kuteketeza kwani huu utaratibu ni endelevu na ili wafanyabiashara wasiweze kuapata hasara ni vyema kuwangalia kila wakati waangalie bidhaa zao na kuhakikisha wanaziuza kabla ya muda au kuwasiliana TBS ili tuviteketeze bure,” alisema Msasalaga.

Aliongeza, “Ukiangalia asilimia kubwa ya bidhaa tulizotekeza ni vyakuka vya watoto hii ina maana tusipokuwa makini tutatengezeza taifa la baadaye lenye matatizo ya kiafya. Hivyo jamii pia inatakiwa kushiriki katika vita hii kwa kukagua muda wa matumizi ya bidhaa wanazo nunua.”

Sheria ya Viwango Namba 2 ya Mwaka 2009 pamoja ya Sheria ya Fedha Namba 8 ya Mwaka 2019, mbali na majukumu mengine zimelipa mamlaka shirika hilo kuondoa bidhaa hafifu sokoni na kuziharibu ama kuzirudisha zinakotoka pindi zinapobainika kuwa hazifai kwa matumizi ya binadamu.

Naye Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano cha TBS, Roida Andusamile alisema wakaguzi wa TBS hufanya ukaguzi wa bidhaa viwandani na sokoni ili kujiridhisha na hali halisi ya soko na inapobainika uwepo wa bidhaa hafifu huondolewa sokoni na aliyekutwa na bidhaa hizo hulazimika kulipia gharama ya uteketezaji.

Aidha, Andusamile ametoa rai kwa wafanyabiashara wote kuhakikisha wanazingatia ubora kwa kuuza biadhaa za vipodozi na vyakula vilivyosajiliwa na ukomo wa matumizi wa bidhaa hizo ili kulinda mlaji na kuepuka hasara ya kuharibiwa bidhaa hizo.

“Pia wafanyabiashara wote wametakiwa kusajili bidhaa za vyakula, vipodozi, majengo ya kyfanyia biashara na maghala ya kuhifadhia bidhaa hizo,” alisema

Naye Mkaguzi wa TBS, Domisiano Rutahala alisema wafanyabiashara wanaouza vipodozi kufuata orodha ya vipodozi ambavyo vimeruhusiwa.

“Ikumbukwe kuwa vipodozi vyenye sumu za hydroquinone, zebaki, madini tembo, na arbutin ambazo zinasababisha kansa za ngozi na kwa wanaotumia muda mrefu wanaweza pata matatizo ya uzazi. Lakini pia kwa upande wa chakuala kinachoishi muda wake kuna kuwa sumu,” alisema Rutahala.

Rais wa Zanzibar, Dk Hussein ...

foto
Mwandishi: Anastazia Anyimike, Dodoma

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi